Na Andrew Mushi KWa muda sasa tangu nimekuwa nikiandika makala na mada nyingine katika vyombo vya habari , nimekuwa nikipokea maoni mengi sana kwa njia ya barua pepe, simu, ujumbe mfupi wa simu na hata ana kwa ana. Wengi wa wanaotoa maoni wanakimbilia kunyooshea vidole viongozi wa vyama vya siasa na zaidi chama tawala, na taasisi nyingine za utawala ndio wanawajibika kuchukua hatua ili kuleta mabadiliko na maendeleo ya nchi yetu. Kitu kimoja kinachojitokeza wazi ni kuwa viongozi ndio wanapaswa kuwa wabunifu, kupangilia vizuri mipango ya maendeleo. Zaidi tegemeo limewekwa kwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na baraza la mawaziri na kwa mbali kidogo wabunge. Kwa mtizamo wangu, hapo ndio tunapokosea. Mbaya zaidi, ni taasisi za kitaifa ndio zinazotazamwa kuwa ndio zenye nafasi ya kuleta mabadiliko. Taasisi kama kijiji, kata au hata wilaya hazionekani kuwa nafasi ya kuwa chachu ya kuleta mabadiliko tunayoyatamani kila kukicha. Pia, kuna asasi na taasisi kama makanisa, misikiti, hospitali,