Kinyozi Mzee kuliko wote...
Hii inaweza kuwa mara ya 300 kwa Mike Jaffe kwenda kunyoa nywele na ndevu kwa Bw. Anthony Mancinelli na pia kupiga blahblah kidogo. Kwa mujibu wa kitabu cha "Guiness Book of World Records", Anthony ndiye kinyozi mwenye umri mkubwa kuliko vinyozi wote duniani. Ukienda kwa Anthony huishii kunyoa nywele peke yake bali utajikuta unaongelea hali ya hewa ya siku hiyo, nani kaja na nani kaondoka mjini, nani kafa nani kazaliwa, na mambo mengine mengi kama hayo. Wateja wa Anthony wanasema mzee huyu ambaye atatizmiza miaka 99 Machi 2 mwaka huu ni sawa na maktaba inayotembea katika jiji la New York huko Marekani. Jamaa alianza kunyoa watu nywele na ndevu akiwa na miaka 12, hii ina maana amepiga kazi ya kinyozi kwa miaka 87. Hii ndio sifa inayomfanya Anthony kuwa kinyozi mzee kuliko wote duniani. Anthony alimwambia Jaffe, "Nilipoanza kazi hii nilikuwa nalipwa senti 5 kwa kichwa". Jaffe amekuwa akinyoa nywele kwa Anthony kwa miaka 25 sasa. "Baadae bei ikapanda kido...