FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016
Nembo ya Shirika la Kimisionari la Bikira Maria Mama wa Yatima. Niliikuta nembo hii nilipoingia nyumba ya Masista wa Shirika hili kwenda kumwona Sista Restuta. Hapa nilipelekwa na Pius baada ya kupata ruhusa ya Mlinzi. Sista Restuta (Mama wa watoto hao) akiwaandaa wanae kuimba nyimbo kituoni hapo. Chakula kilichoandaliwa na familia yangu kwa ajili ya watoto hao Sehemu ya kukaa wageni na watoto wa kituo cha Furaha Mbweni Kijijini. Watoto wakichukua chakula. Sister Restuta na utawala wa kituo umeweka utaratibu mzuri sana wakati wa kula. Wanaanza watoto wa Chekechea (Nursery School), wakifuatia wa Shule ya Msingi kuanzia darasa la Kwanza kuendelea mpaka Kidato cha Sita. Kituo hiki kunachukua watoto wa kuanzia miaka mitatu ambao wanasoma Chekechea Watoto wakiendelea kuchukua chakula Huyu mtoto wa kushoto mwenye fulana nyeupe anaitwa Pius. Alinipokea siku moja kabla nilipokwenda kupeleka vyakula vyao na kufanya maandal...