THE SECRET BEHIND HIDDEN POWERS.!!!
By My Friend (Name WITHHELD), Mwaka 1836 binti mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 18 kutoka familia ya kitajiri huko Lexington, Kentucky alimuomba Mungu aolewe na Rais wa Marekani. Licha ya kwamba utajiri wa familia yao ulitokana na biashara ya utumwa lakini wazazi wake waliamua kuachana na biashara hiyo mwanzoni mwa miaka ya 1800's na kuwa wacha Mungu. Mary alikuwa muumini wa makanisa ya uamsho kwa wakati huo (Presbyterianism), kama ilivyo makanisa ya kiroho leo. Siku moja akamwabia baba yake, "Mungu ameniambia kuwa mwanaume wa maisha yangu atakuwa Rais wa nchi hii". Baba yake akastaajabu, lakini hakutaka kumkatisha tamaa. Akamwambia "binti yangu, nchi hii ni kubwa sana, na wasichana wengi wangependa kuolewa na watu mashuhuri na wenye madaraka, lakini si jambo rahisi kuolewa na Rais. Na ukisubiri hali hiyo kutokea unaweza usiolewe kabisa katika maisha yako". Lakini yule msichana akamtizama baba yake kisha akamjibu "sijali ni wasichana wa...