TANZIA - KANALI MSTAAFU SAMWEL ELIEZER MOSHA (P1397)
Kuzaliwa 06 JAN 1944 - Kufariki 01 DEC 2017 Mzee wetu huyu amelitumikia Jeshi la Wananchi la Tanzania katika nafasi mbali mbali mpaka anastaafu Jeshi Tareh e 24 SEP 1983 alikuwa na cheo cha Kanali. Amewahi kuwa 'field engineer' na 'inspector' huko Jeshini , amekuwa mwalimu wa maaskari Chuo cha Jeshi Mond uli, amekuwa Mwalimu wa wapigania Uhuru mbali mbali wa Afrika huko Nachingwea Tanzania. Ni rafiki na Mh. Yoweri Kaguta Museveni (Rais wa Uganda) na alikuwa rafiki na Hayati Samora Machel (Aliyekuwa Rais wa Msumbiji). Amepigana vita ya Uganda, baada ya vita ya Uganda alikuwa Msaidizi wa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Amekuwa pia Mkuu wa Wilaya mbali mbali kipindi cha awamu ya Kwanza ya Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Amekuwa pia Mkurugenzi kwenye Shirika la Bima la Taifa (NIC) kabla ya kustaafu rasmi kwa mujibu wa sheria. Kanali Mstaafu Samwel E. Mosha alikuwa ni ndugu (rika moja) na Marehemu Baba Yangu Mzazi ...