TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE 1. Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote, Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana Nilalapo nakuwaza wewe, niamkapo ni heri mama wee Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote. 2. Tanzania Tanzania, ninapokwenda safarini, Kutazama maajabu, biashara nayo makazi, Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu hakika Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote. 3. Tanzania Tanzania, watu wengi wanakusifu, Siasa yako na desturi, ilituletea uhuru Hatuwezi kusahau sisi, mambo mema ya kwetu hakika Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote. Swali, Je leo hii tunaweza kusimama na kuimba wimbo huu, tukiwa kifua mbele na furaha kama enzi zile? nahisi umaarufu wa wimbo huu umepotea, hata mashuleni sidhan kama unaimbwa tena, au na wenyewe ulikuwa ndani ya kale kakitabu ka AZIMIO LA ARUSHA. Naomba kuwakilisha...