Huo ni mchemsho wa kuku na chai au kahawa... hii ilikuwa jioni siku niliyoingia Singida rasmi. Hapo ni Lake Hill Hotel, iliyopo kilimani. Kuku choma ikiwa katika maandalizi, juu na chini... hapo ni iliyokuwa NBC Club, Singida. Baada ya kuku kuiva, ikiwa mezani tayari kuliwa juu na chini. Hii ni nyama choma na kuku choma kwa ugali. Hapo ni Kirima Hapo ni mnadani, nyama choma ikiandaliwa na chini ikiwa tayari mezani kwa kuliwa... Mnada huwa unanoga sana, hasa kwa upande wa nyama choma... juu na chini... Kuku choma jioni moja pale Mbacho... Baada ya msosi, siku moja moja unashushia kutumia mvinyo... glasi moja ya mvinyo ni kama dawa. Husaidia kuondoa "kolestro", kuyeyusha chakula, nk... Asubuhi kuna supu safi sana ya kuku (Singida kuku ni wa kienyeji tuu) na chapati. Hii ilikuwa Pale Lutheran Hostel. Mzee Wilson "Machare" Mosha ndio kijiwe chake kila mara akiwa Singida ...