Leo nimeamua kutoa mtazamo wangu kuhusu uwekezaji unavyofanyika hapa nchini kwetu. Kwasababu uwekezaji ni hoja pana (mtambuka) na yenye kuhitaji utaalamu wa sekta mbali mbali, mimi nitatoa mtazamo wangu binafsi kwa namna nilivyoona mimi, kwa kutumia uwekezaji wa Dangote Industries kule Mtwara. Kwanza kabisa bila kumung'unya maneno nakubali kabisa kwamba uwekezaji ule ni MUHIMU sana kwa uchumi wetu na watanzania kwa ujumla. Ni suala la msingi na linalohitaji kupongezwa. Pamoja na hayo, kuna changamoto zinazojitokeza kwenye kila shughuli. Kwa uwekezaji huu wa Dangote Industries, mimi nimeona changamoto zifuatazo. Mwekezaji hakutakiwa kupewa gesi ili yeye atumie kuzalishia moja kwa moja umeme wake, nishati ya mitambo na reli ya kuingiza malighafi kiwandani na kutolea cement baada ya uzalishaji. Hapa namaanisha kwamba hakutakiwa kupewa bomba lake peke yake ili yeye azalishe umeme, nishati ya uzalishaji na uendeshaji wa mitambo, kujenga reli yake mwenyewe kuleta mali ghafi kiwa