Tujifunze kushukuru kwa kila kitu!

Kijana mmoja aliyekuwa akijiandaa kwa mahafali ya kuhitimu chuo kikuu, kwa muda mrefu alikuwa akiitamani gari moja ya kifahari ya kimichezo iliyokuwa ikiuzwa katika duka moja la magari, na akijua dhahiri kuwa baba yake ana uwezo wa kununua gari hilo na kumpa yeye kama zawadi yake kwa kuhitimu masomo vyema, na alimwambia baba yake kuwa hicho ni kitu alichokipenda mno. Kadri siku zilivyokuwa zikisogea kuelekea mahafali kijana huyo alisubiri kwa hamu kuona dalili za baba yake kumnunulia gari hilo. Siku ya siku ikafika na asubuhi ya siku hiyo ya mahafali, baba yake alimwita kwenye chumba chake cha kusomea na kumwambia ' Najivunia kuwa na mtoto bora kama wewe' na pia akamwambia ni kwa kiwango gani anampenda. Akamkabidhi kijifurushi cha zawadi kilichofungwa vema kwenye karatasi safi za kufungia zawadi. Akiwa mwenye hamu kubwa lakini akiwa amekatishwa tamaa alifungua kifurushi hicho na kukuta ni Biblia nzuri yenye jalada la ngozi na juu yake kumeandikwa jina la kijana huyo kwa maandishi nadhifu yaliyonakshiwa kwa dhahabu. Kwa hasira akamfokea baba yake akisema ' Yaani pamoja na pesa zako zote unanipa biblia?'akatoka hima ndani ya nyumba hiyo na kuiacha biblia.

Miaka mingi ikapita na kijana akawa ni mtu wa mafanikio sana kibiashara. Alikuwa na nyumba nzuri na familia bora, lakini akagundua baba yake ni mzee sana sasa, na akadhani ni muhimu kwenda kwake. Na alikuwa hajawahi kumuona tena toka siku ile ya Mahafali. Kabla mipango yake haijatimia, akapokea waraka wa simu ukimtaarifu kuwa baba yake amefariki dunia, na amemrithisha kila kitu alichokuwa nacho kijana wake wa pekee. Hivyo alitakiwa kurudi nyumbani haraka kusimamia mali za baba yake.

Alipofika nyumbani kwa baba yake , alipata uchungu na majuto ya hali ya juu rohoni. Akaanza kupekua baadhi ya nyaraka muhimu za baba yake ndipo! alipoikuta ile biblia ikiwa vile vile kama alivyoiacha miaka kadhaa nyuma. Huku akilia alifungua kurasa za biblia. Baba yake kwa umakini mkubwa alipigia mistari maneno yaliyopo katika Mathayo 7:11, yanayosema ' basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema,je! Si zaidi sana Baba yenu aliye Mbinguni atawapa mema wao wamwombao?. Wakati akisoma maneno hayo, funguo za gari zikadondoka kutoka katika kurasa za mwisho za biblia. Ikiwa na jina pamoja na alama ya lile duka la kuuza magari ya kifahari ya kimichezo aliyokuwa akiyapenda sana. Kukiwa na tarehe ile ya siku yake ya mahafali huku imeandikwa ... IMELIPIWA PESA KAMILI.

Mara ngapi tumezikosa baraka za mwenyezi mungu eti kwa sababu hazijafungwa tutakavyo? Naamini umefurahia hili somo la leo. Peleka ujumbe huu kwa wengine. Usipoteze ulichonacho kwa kutamani usichonacho: Lakini kumbuka ulichonacho sasa ni moja kati ya vitu ulivyo vitamani huko siku za nyuma. IKIWA ZAWADI UPEWAYO HAIJAFUNGWA KWA KADRI UTAKAVYO, NI KWA SABABU HIVYO NDIVYO HALI BORA KABISA YA UFUNGWAJI WAKE ULIOPATIKANA! SIKU ZOTE SHUKURU VITU VIDOGO: KWANI HUWA NA VITU VINGINE NDANI YAKE!

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Taarifa za msiba...