Changamoto kwa vyombo vya usalama Bongo...
Nimekuwa nafikiria mambo mbali mbali yaliyotokea nchini haswa yanayohusu usalama wa mtandao , mwaka huu kumeripotiwa na magazeti kadhaa kukamatwa kwa watu waliokuwa wanaiba kwa njia ya mtandao katika benki ya BACLAYS ingawa Waandishi wale walikuwa hawajabobea katika masuala waliyokuwa wana ripoti kama hili na Kibaya zaidi jumuiya za mambo ya ICT Tanzania hata hawakukutana kuongelea changamoto hii hata kufanya mdahalo wa wazi kwa faida za umma .
Likaja suala la wizi wa kutumia ATM kwa bahati mbaya wakati ule niliwahi mimi mwenyewe binafsi nikatoa taarifa Fulani hivi pamoja na hili kuna watu Fulani Fulani nililazimika kukaa nao vikao kuongelea suala hili kwa mapana zaidi ukiacha wale wa vyombo vya habari , nalo hili wadau wa secta ya benki hawakutoa taarifa za ziada kwa wananchi sijui sasa tuwaeleweje .
Kabla ya matukio haya mawili kuna wakati Fulani kuanzia mwaka jana kuna genge la watu waliokuwa wanaiba account za wateja mbali mbali wa TTCL na kampuni zingine zilizokuwa zinatoa huduma ya Internet , hii nayo ilikuwa siri mpaka wengine wajitolee wapepeleze wapate majibu ndio wayapeleke kwa hao wenyewe TTCL , Wakati wenyewe unakuta walishatafuta mkandarasi mwingine toka ulaya aje kuangalia mfumo wao awarekebishie mambo .
Baada ya TTCL kutumia pia hizo gharama za ziada kualika wataalamu wa kuja kutoa ushauri na kutatua tatizo hilo , bado genge hilo likaja na njia zingine likaendelea kuiba account hizo , lakini alipatikana Yule kigogo wao aliwekewa mtego akaenda kuingiza account zake mwenyewe ndio hapo ukawa mwisho wake .
Fikiria Kampuni kama TTCL inawateja wangapi Tanzania hii ? imeshindwa kutoa taarifa ndogo tu kuwaelezea wateja wao kwamba kuna hili na lile linaendelea kwahiyo unachotakiwa ni kufanya hivi na hivi mfano badilisha pwd ya account yako , uwe unakagua account yako kila baada ya muda Fulani , omba matumizi ya account yako toka kwa offisi zetu mara kwa mara hili nalo lilishindikana .
Kama nilivyokwambia hapo juu ni watu wachache wazalendo wanaona vitendo hivi vinaendelea wanaamua kwa moyo wao mmoja bila malipo yoyote kufanya upelelezi wao kuwafikia magenge haya , kunukuu matendo yao wanayoyafanya na kisha kuwazima kimya kimya na kufanya hii siri wengine wanaogopa kuwasiliana na kampuni hizi pengine unayewasiliana nae ndio kakake Yule mhalifu .
Kwa kuwa kumekuwa na matukio ya kihalifu mara kwa mara natoa rai kwa wadau mbali mbali katika majukwaa mbali mbali ya mitandao wawe wanaandika kuelezea japo mistari michache kuhusu wanachojua wao ili iwe rahisi kushugulikia baadhi ya vitu kwa kasi zaidi na kwa wepesi zaidi .
Mimi binafsi nimeanza muhula huo kama unavyoona chochote ambacho kipo kinaendelea napenda kusema japo mistari michache hata kama ni kwa lugha ya kigeni angalau wananchi wajue kinachoendelea katika mipaka yetu na nje ya mipaka hii .
Ni jukumu la kila mwananchi mzalendo wa nchi hii kuhakikisha usalama katika mitandao yetu haswa ya ndani unakwepo na kutoa taarifa za haraka na ukweli kuhusu vitendo vinavyoendelea ambavyo vinadidimiza maendeleo ya nchi .
Vyombo vya usalama pamoja na jeshi la polisi nalo lianzishe vitengo maalumu vya kupokea taarifa hizi pamoja na mijadala mengine inayoendelea ili view updated kila mara ni maajabu kwamba taarifa kama ile ya Mgeni kule AirPort vyombo hivi vilishindwa kupata mapema .
Niliwahi kushauri maeneo ya kati kati ya jiji kama Mtaa wa Jamhuri na Mkwepu pamoja na kariakoo kuwe na Mitandao maalumu ya kufuatilia baadhi ya vikundi vya watu , tunajua kariakoo ni mbingu ya vyeti , temeke ni mbingu ya kutengeneza cd pamoja na makasha bandia , jamhuri ni masuala ya kuforge na vitu kama hivyo .
Siku hizi kuna matangazo ya kazi yanatolewa kama njugu kwenye mitandao mengine yanakuwa ni hadaa , hata kama mtu anafanikiwa kutoka hapa huko anapoenda ndio anaenda kupata cha mtema kuni hivi vyote ni vitu vya kuangalia na kujadili pamoja .
Kuna kampuni na watu binafsi wanauza programu ambazo ni bandia kwa makusudi watu hawaulizi wala kuhoji chochote , ilimradi ameshapata kiten percent chake hana mpango na wengine , mashambulizi mengi ya virus na spyware kwa siku za karibuni yametokea huko .
Kwa mtindo huu inawezekana kabisa wahalifu wakafanya nchi yetu kama sehemu yao ya kuanzisha mashambulizi kwenda sehemu zingine kama vitu vikiendelea kuwa kama hivi ilivyo , yaliyotokea korea kusini na marekani mwezi uliopita iwe ni funzo hata sisi kwetu
Source: JamiiForum

Comments