Wachawi wanachomwa LIVE!!!
KATIKA MAZINGIRA KAMA HAYA, UNAMCHOMA MWENZAKO KAMA KUKU, USHAHIDI HUNA... HATA KAMA UNA USHAHIDI, ZIPO TARATIBU ZINAZOKUBALIKA KIKATIBA NA KISHERIA ZA KUSHUGHULIKIA WATU WOTE WANAOKIUKA UTARATIBU TULIOJIWEKEA KUISHI KATIKA JAMII YETU. NI KUWAFUNGULIA MASHITAKA NA MAHAKAMA ITOE HUKUMU.
INAWEZEKANA KABISA MTU AKACHOMWA KWA TUHUMA ZA UCHAWI, NA ASIWE MCHAWI. TUMEONA BIBI WAZEE WAKISINGIZIWA UCHAWI KWA RANGI YA MACHO YAO, WAKATI SABABU ZA UKWELI NI MAZINGIRA WANAYOISHI YA KUTUMIA JIKO LA KUNI NA KUPULIZA MOTO MIAKA NENDA RUDI TANGU USICHANA MPAKA UZEE. LEO UNAMCHOMA MOTO AU KUMKATA NA MAPANGA ETI MACHO MEKUNDU, HIVYO MCHAWI.
HAWA BIBI ZETU NDIO HAWA HAWA WALIOTAABIKA KUTULEA, AU KUWALEA WALITUTANGULIA. UTARATIBU WA KUHESHIMIANA NA KUVUMILIANA UMEKWENDA WAPI WATANZANIA WENZANGU?
JAMANI, TUNAMWOGOPA MUNGU KWELI... HEBU TUTAFAKARI NA KUJITAFAKARI KWA KINA. IMENIUMA SANA. TUJITAHIDI TUSIBURUZWE NA WACHACHE KWENYE MAAMUZI MAGUMU YATAKAYOTUFANYA KUJUTA SANA. TURUDISHE UVUMILIVU WETU NA KUHESHIMIANA, NAWASIHI. KICHWAGUMU.
Comments