Mtoto aadhibiwa kwa kunin'ginizwa mtini kichwa chini miguu juu!
Dickson Mjarifu, mtoto wa miaka minane tu, mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Dukamba, amepewa adhabu ya kuning’inizwa mtini miguu juu kichwa chini angali amefungwa miguu na mikono yake. Mtoto huyo mkazi wa kijiji na kata ya Kharumwa wilayani Geita alipewa adhabu hiyo kwa karibu wiki moja na mama yake wa kufikia, Dafroza Masilu (25) kwa kushirikiana na baba yake mzazi, Hezron Mjarifu (35) na kuonywa kuwa angethubutu kusema lolote kuhusu adhabu hiyo, basi angeuawa. Akisimulia kisa hicho mwanzoni mwa wiki hii katika mahojiano maalumu na gazeti la Serikali la HabariLeo, mwalimu wa darasa analosoma mwanafunzi huyo, Agnes Boniphace, alidai kuwa Alhamisi iliyopita muda wa Asubuhi, wanafunzi wenzie Dickson walitoa taarifa shuleni kuhusu mateso aliyokuwa akipata mwenzao. Kwa mujibu wa Mwalimu Agnes, ambaye sasa anaishi na Dickson, wanafunzi hao walipokuwa wakipita njiani karibu na nyumba anayoishi mtoto huyo, Dickson aliwaita kuwaomba msaada. ...