This Blog History...

Wadau wapendwa, 

Leo ni miaka kadhaa tangu kuanzishwa kwa blogu hii. Wengi wenu hamjui kilichosababisha kuanzishwa kwa blogu hii, yaani "secret behind this blog" kwa ufupi sana ni kwamba, leo ni siku ya kuzaliwa Hayati Baba yangu Mzee Alfred S. S. Mosha alizaliwa tarehe 3 mwezi wa 3 mwaka 1944 na kufariki tarehe 2 mwezi wa 9 mwaka 1994. Wakati huo huo, "Office Mate" wangu mpenzi sana, Da' Chiku Haidari, Leo pia ni siku yake ya kuzaliwa. 

Sasa, siku ilipoanzishwa blogu hii, ilikuwa siku kama ya leo miaka kadhaa huko nyuma. Nilifika ofisini kama kawaida, nikijua leo ni B'day ya Mzee wangu na wakati huo huo ni B'day ya Da' Chiku. Nikafikiria kitu cha kuweza kufanya kama "suprise" kwa chiku bila kumwambia na wadau wengine wa ofisi waweze kujua B'day hii ya chiku, kawaida Da' Chiku ni mkimya sana na asiyependa kusumbua watu kwa kuwajulisha mambo yake. 

Nikaingia kwenye mtandao nikitaka kutuma 'e-card with a present' kule nikakuta zile zawadi za maana lazima ununue, mimi sina 'e-wallet'. Lakini katika ku-peruse mtandao ndio nikakuta uwezekano wa kufungua blog! Nikasema hapa-hapa. Nikaisajili blogu hii, na post ya kwanza ilikuwa "B'day ya Chiku Haidari". Nikamtakia heri katika siku kuu yake ya kuzaliwa na ndio ukawa mwanzo wa blogu hii. Baada ya muda nikafungua nyingine inayoitwa 'http://bongotambarare.blogspot.com'.

Ukitaka kuthibitisha haya maneno, tafuta post ya kwanza kabisa kwenye blogu hii, na utaamini nikwambiacho. 

Kwa mtazamo huo huo, LEO TENA, NAKUTAKIA HERI YA KUZALIWA DA' CHIKU HAIDARI NA KUKUOMBEA KWA MWENYEZI MUNGU UBARIKIWE SANA NA UZIDI KUFANIKIWA, AMEN. 

KICHWANGUMU.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Taarifa za msiba...