Kutoka Namanga njiani kurudi Arusha tumekuta fisi akiwa amegongwa maeneo ya Ingikaret. Fisi huyo aina ya 'stripped hyena' huwa si maarufu sana kama wale waliozoeleka wa 'spotted hyena'.
Nembo ya Shirika la Kimisionari la Bikira Maria Mama wa Yatima. Niliikuta nembo hii nilipoingia nyumba ya Masista wa Shirika hili kwenda kumwona Sista Restuta. Hapa nilipelekwa na Pius baada ya kupata ruhusa ya Mlinzi. Sista Restuta (Mama wa watoto hao) akiwaandaa wanae kuimba nyimbo kituoni hapo. Chakula kilichoandaliwa na familia yangu kwa ajili ya watoto hao Sehemu ya kukaa wageni na watoto wa kituo cha Furaha Mbweni Kijijini. Watoto wakichukua chakula. Sister Restuta na utawala wa kituo umeweka utaratibu mzuri sana wakati wa kula. Wanaanza watoto wa Chekechea (Nursery School), wakifuatia wa Shule ya Msingi kuanzia darasa la Kwanza kuendelea mpaka Kidato cha Sita. Kituo hiki kunachukua watoto wa kuanzia miaka mitatu ambao wanasoma Chekechea Watoto wakiendelea kuchukua chakula Huyu mtoto wa kushoto mwenye fulana nyeupe anaitwa Pius. Alinipokea siku moja kabla nilipokwenda kupeleka vyakula vyao na kufanya maandalizi ya siku hii rasmi. A
Kwa masikitiko makubwa nawataarifu msiba mkubwa tulionao leo. Ndugu yetu, mpendwa wetu, mwenzetu kwenye TEKNOHAMA na mdau mkubwa wa tafiti mbali mbali za TEKNOHAMA Kaka Andrew dACHI amefariki leo asubuhi nyumbani kwake Fransic Town, Botswana. Kwa sasa sina la ziada, ila tutaendelea kupeana taarifa kadri zitakavyotufikia. Tunaungana na familia yake, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo, kumwomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi, wakati taratibu za mazishi zinafanyika. Bwana alitoa, nae ametwaa. Jina lake lihimidiwe. tunaweza kujikumbusha moja ya kazi zake kwa kufungua ' http://www.isaconsulting.biz /' email yake ilikuwa ' andrew.dachi@isaconsulting.biz '
Comments