Berlusconi story...
Na David 'Bob' Mosha,
DSM.Daktari anayemtibu Waziri Mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi, amesema kuwa waziri huyo kwa sasa hawezi kuruhusiwa mpaka angalau Jumatano. Pia ameeleza kuwa waziri huyo ameweza kula japo kwa shida.
Berlusconi, mwenye umri wa miaka 73, alipata jeraha puani, kuvunjwa meno mawili na jeraha mdomoni baada ya kushambuliwa kwa kutumia sanamu moja lenye umbo la Kanisa Kuu la mjini Milan. Bwana Massimo Tartaglia, 42 anashikiliwa kuhusika na tukio hilo.
Zifuatazo ni picha za tukio hilo lilivyokuwa:

Massimo Tartaglia (mtuhumiwa) akimshambulia waziri huyo.
“Bwana mkubwa” alikuwa hivi baada ya kipondo kutoka kwa Massimo.
Mtuhumiwa akiwa “mtu kati” kuzuia kushushiwa kichapo na raia wenye hasira.
Kigogo huyo wa kitaifa akiweweseka baada ya kukumbana na dhoruba hiyo.
Berlusconi akipewa huduma ya kwanza kabla ya kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Hii ndiyo sanamu aliyogongwa nayo kigogo huyo baada ya kushambuliwa na Massimo.
Comments