Na Chrizant Kibogoyo KUTOKANA na wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji na mitaa kushindwa kutumia sheria nzuri zilzizopo kulinda maslahi ya wananchi katika ardhi, Watanzania wanatakiwa kufuata nyayo za hayati Mwalimu Nyerere aliyetangaza hadharani kumuunga mkono na kisha kumpigia kura mgombe wa NCCR Ndg Paul Ndobo kwa ajili ya Ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mwaka 1995 na kumuacha mgombea wa CCM aliyekuwa na tuhuma za kufilisi ushirika. Ikiwa hayati Mwalimu Nyerere muasisi wa TANU na baadaye CCM aliweza kutambua umuhimu wa kuweka maslahi ya nchi mbele kabla ya maslahi ya chama chake cha CCM kwa kuchagua kiongozi bora na sio bora kiongozi kwa kuwa katoka CCM. Mwaka 2009 na 2010 Watanzania wanatakiwa kuamka na kutumia vyema haki zetu za kikatiba kuchagua timu ya viongozi ambao watakwenda kuweka maslahi ya taifa mbele na sio maslahi ya vyama na binafsi Bungeni. Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999 imeanda utaratibu muafaka na shirikishi kweli kweli wa kuingiza eneo katika MPANGO WA URASI...