Uvivuzzzzzzzz!

Fuatilia huu mjadala:
Kijana: Baba naomba glasi moja ya maji ya kunywa
Baba: Si uchukue mwenyewe, wee kichaa nini?
Kijana: Jamani baba, si nimekuomba lakini?
Baba: Ukisema tena ntakuja hapo ulipo kukuzaba kibao.
Kijana: Basi ukija kunizaba kibao uje na maji ya kunywa pia.
Mwingine huu hapa:
Daktari: Vipi nini tatizo la jicho lako?
Mgonjwa: Jicho limeingiliwa na tope.
Daktari: Tope? Imekuwaje?
Mgonjwa: Mie naishi kwenye nyumba yenye paa la udongo, nikiwa nimejipumzisha chali sebuleni huku natizama dari mida ya mchana. Mara ghafla mvua ikaanza kunyesha na paa langu linavuja. Nikawa naona uvivu kufunga jicho tope taratibu ndiyo likajaa jichoni.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.