Chips Kuku za Moshi Town @ Vunjo Bar...

 Hii ni kuku ndizi...
 hii ni kuku pekee... juu na chini.

 mlango wa kuingilia 'restaurant' baada ya kuweka 'order' yako hapo nje...
 sehemu ya maandalizi ya kuku, viazi na ndizi...
 wateja wakiweka order zao jikoni
 bidhaa a.k.a mzigo  ukiwa jikoni kwenye maandalizi...
 kul boksi ya kuhifadhia kuku baada ya kukaangwa kabla ya kuuzwa!


 Mlango wa kuingilia Vunjo Bar...

 chips kuku ikiwa tayari kwa kuliwa, mhudumu wa siku hiyo akionekana chini...
Hapo Vunjo Bar ni muungano wa wakina mama wajasiriamali waliamua kukaa pamoja kuweka mitaji kufuga kuku na kuwauza. Kuna kuku wazuri, waliofugwa kwa ustadi mkubwa na wanaondaliwa vizuri sana. Nilikula robo kuku, kutokana na ladha nzuri au tamu ya kupindukia nililazimika kuongeza kuku. Wenyewe wanasema kama ukihitaji kuongeza chips ni bure, ila kuongeza kuku nalipa. Nakuhakikishia ukienda lazima utaongeza kuku!

kwa wakina mama ambao hawana mtaji kwenye kundi hilo, wao hutoa mtaji wa nguvu kazi kwenye maandalizi ya milo hiyo. Biashara hii ipo kwenye nyumba ya mmoja wa akina mama hayo. Kwa kweli wanastahili pongezi kwa namna walivyojipanga.

wametengeneza ka-mzunguko kazuri ka kuuzia kuku zao. HONGERENI SANA...

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.