Wawindaji wapigwa risasi Selous, Ephraim Mkenda wa Miller Bar, Sinza Mori alikuwepo.

Watu wawili wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupigwa risasi na askari wa wanyamapori wa Pori la Akiba la Selous.
Watu hao waliokuwa na kibali cha kuwindia walikutwa na mkasa huo juzi jioni katika eneo la wazi la Utete, Rufiji baada ya askari wa Selous kufyatua risasi wakidhani ni majangili waliotoka katika pori hilo.
Akizungumza na gazeti hili jana, mwindaji Mashaka Ndonde alisema alikuwa amekwenda na rafiki zake kuwinda nyumbu katika eneo hilo, lakini ghafla wakati wanaondoka na mnyama huyo saa 12:30 jioni walisikia sauti ikiwaamuru kusimama.
“Wakati bado tunashangaa tukasikia risasi imelia iliwapiga watu wawili, mmoja ni rafiki yangu alikuwa amekuja kunisindikiza anaitwa Ephraim Mkenda na mwingine ni mwongozaji kutoka Kijiji cha Utete, Malick Sadick,” alisema Ndonde.
Alisema kuwa askari hao waliokuwa na sare za kazi na bunduki, waliwashusha kwenye gari na kuwalazimisha wawafuate kinyumenyume.
“Tukawaambia sisi ni wawindaji halali, wakatulaza chini hadi giza lilipoingia. Walisikika wakisema lazima watuue. Nikawaambia mkituua hamuwezi kupoteza ushahidi kwa sababu wenzetu wawili wamekimbia,” alisema Ndonda.
Aliongeza kuwa, baada ya askari kubaini kuwa wawindaji walikuwa saba na kwamba wawili walifanikiwa kuingia porini, ndipo walipoamua kuwaruhusu kuondoka huku wakiwataka wasiseme kilichowakuta.
Wakati wakiondoka eneo hilo walikutana na Ofisa Mhifadhi wa Wilaya ya Utete, Edd Kilapilo na kumwelezea namna walivyonusurika kuuawa na askari wanyamapori.
Alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, Kilapilo alimtaka mwandishi kuyaamini maneno ya watu waliojeruhiwa kwa kuwa wao ndiyo wanajua nini kimewapata.
Alipoulizwa iwapo ana taarifa za tukio hilo alisema: “Kwa kifupi nimesikia watu wawili wamepigwa risasi huko porini, basi.”
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei alisema alimtuma Mkuu wa Polisi wa Wilaya kwenda katika eneo la tukio kujua nini kilitokea. Hadi jana jioni alikuwa bado hajapata taarifa
Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Wawindaji-wapigwa-risasi-Selous/-/1597296/2475796/-/ftplvw/-/index.html 
============================
Bado tunaendelea kufuatilia, tutawapa taarifa zaidi...

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.