THE SECRET BEHIND HIDDEN POWERS.!!!
By My Friend (Name WITHHELD),
Mwaka 1836 binti mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 18 kutoka
familia ya kitajiri huko Lexington, Kentucky alimuomba Mungu aolewe na Rais wa
Marekani. Licha ya kwamba utajiri wa familia yao ulitokana na biashara ya
utumwa lakini wazazi wake waliamua kuachana na biashara hiyo mwanzoni mwa miaka
ya 1800's na kuwa wacha Mungu.
Mary alikuwa muumini wa makanisa ya uamsho kwa wakati huo
(Presbyterianism), kama ilivyo makanisa ya kiroho leo. Siku moja akamwabia baba
yake, "Mungu ameniambia kuwa mwanaume wa maisha yangu atakuwa Rais wa nchi
hii".
Baba yake akastaajabu, lakini hakutaka kumkatisha tamaa.
Akamwambia "binti yangu, nchi hii ni kubwa sana, na wasichana wengi
wangependa kuolewa na watu mashuhuri na wenye madaraka, lakini si jambo rahisi
kuolewa na Rais. Na ukisubiri hali hiyo kutokea unaweza usiolewe kabisa katika
maisha yako".
Lakini yule msichana akamtizama baba yake kisha akamjibu
"sijali ni wasichana wangapi wanaotamani kuolewa na watu mashuhuri, sijali
nchi hii ni kubwa kiasi gani. Ninachojali ni kuwa Mungu ameniambia kuwa siku
moja nitakuwa first lady wa nchi hii. Hilo tu"
Maka mmoja baadae (1837) yule binti akachumbiwa na mwanasiasa
machachari chipukizi aliyekuwa mwanasheria na mbunge wa Illinois (the rising
young lawyer and Democratic Party politician) aitwaye Stephen Douglas. Kwa kuwa
Stephen alikuwa mbunge, baba wa yule binti aliamini kuwa huyo ndiye angemuoa
mwanae na angekuja kuwa Rais wa Marekani baadae. Kwahiyo ndoto za binti yake
zingetimia kupitia Stephen.
Lakini miaka miwili baadae (1839) uchumba wao
ukavunjika.
Mwaka huohuo (1839) katika mji wa Springfield, Illinois,
yule binti akakutana na kijana mmoja msomi wa sheria lakini kutoka familia
maskini huko Indiana. Kijana huyu alikuwa amekuja Illinois kutafuta kazi.
Wazazi wake walikua wakulima maskini. Ardhi yao huko Kentucky ilitaifishwa na
hivyo wakahamia Indiana.
Kijana huyu akapendana na yule binti na kuamua kuoana. Mwaka
1840 mwezi December kijana akamvisha pete ya uchumba yule binti. Baba wa binti
hakufurahishwa. Akajiuliza iweje mwanae amkatae "mbunge" na akubali
kuolewa na "mtoto wa mkulima??". Kwa masikitiko akamuuliza binti yake
"unakumbuka ahadi ya Mungu kwako?". Binti akajibu "hata sasa
bado naamini."
Miaka minne baadae (1843) wakafunga ndoa.
Miaka 17 baadae (1861) yule kijana akachaguliwa kuwa Rais wa
16 wa Marekani. Jina lake aliitwa Abraham Lincoln, na mkewe aliitwa Mary Todd
Lincoln.
Mary ndiye aliyekataa kuolewa na Steven Douglas (Mbunge) kwa
ajili ya Lincoln (mtoto wa mkulima).
Baba yake Marry akiwa mzee wa zaidi ya miaka 80 alishuhudia
mwanae akiwa "First Lady" akamwambia "Mungu wako ni mkuu sana.
Aliahidi na ametimiza". Mwaka mmoja baadae (1862) mzee Robert Todd (baba
yake Mary) akafariki.
MORAL OF YHE STORY.!
Hadithi hii ni ya kweli kabisa inayomhusu Rais Abraham
Lincoln na mkewe Mary Todd Lincoln. Kuna mengi ya kujifunza kwenye kisa hiki,
lakini ningependa kukushirikisha machache niliyojifunza mimi.
#Lesson_1: Ukiomba usichoke kusubiri. Mungu akisema atakupa,
basi amini atakupa tu. Mungu wetu ni mwaminifu na hutupa kwa wakati wake. Mary
aliona maono ya kuwa first lady akiwa na miaka 18, lakini ilimchukua robo karne
(miaka 25) hadi maono yake kutimia. Sasa wewe ndugu yangu umemaliza chuo mwaka
jana umeomba kazi hata mwaka haujaisha umeshaanza kumlalamikia Mungu. Subiri.
Au umeomba mchumba mwaka wa 3 hujapata, unaanza kumlalamikia Mungu eti wenzio
wote wameolewa/kuoa. Tafadhali subiri. Mungu atakupa kwa wakati wake
unaofaa. Ila jishughulishe na kazi halali za ubunifu ili kujijenga, kujipatia kipato halali na kutatua changamoto za jamii inayokuzunguka.
#Lesson_2: Ishi katika misimamo. Baba yake Mary Todd
alipoona mwanae amemuacha "Mbunge" akaolewa na Mtoto wa mkulima
alimuona kama vile amepoteza dira. Lakini binti alijua ipo siku Mungu atatenda.
Na Mungu alivyo mwaminifu hakumruhusu baba yake Mary kufa kabla hajashuhudia
Mwanae akiwa "first lady" wa Marekani. Point hapa ni kwamba jifunze
kushikilia imani yako na uwe na msimamo usioyumba hata kama dunia nzima
itakuacha. Wengi waliobarikiwa ni wenye misimamo. Jifunze kuwa focused and
visionary. Usitazame vinavyong'ara leo, tazama vitakavyong'ara milele.
#Lesson_3: kuna kitu kinaitwa "Hidden Power" yani
nguvu iliyofichwa. Ni nguvu ambayo unakuwa nayo wewe lakini inatokana na watu
wengine. Unaweza kufanikiwa sana, lakini si kwa juhudi zako bali kwa sababu
nyuma yako kuna watu wanaofanya wewe ufanikiwe. Wanakuombea, wanafunga kwa
ajili yako, wanamsihi Mungu kwa ajili yako, wanaomba ulinzi, baraka, na neema
kwako. Wanaweza kuwa wazazi wako, mwenzi wako, watoto wako, rafiki zako, ndugu
zako etc.
Lincoln alikuwa na nguvu iliyofichwa kupitia mkewe. Yani mke
wa Lincoln (Mary) ndiye aliyemfanya mumewe kuwa Rais (Mary was focused, determined with a clear vision and purpose). Kama Lincoln asingemuoa
Mary Todd asingekuwa Rais wa Marekani. Na hata Lincoln mwenyewe aliwahi kukiri
kwamba "Urais haukuwahi kuwa ndoto zake katika maisha"
#Lesson_4: Our GOD is the GOD of miracles. Yale
tunayoona na kudhani hayawezekani, kwa Mungu yanawezekana. Wakati Mary akiwaza
atakuwa first lady wa Marekani, Lincoln hakuwahi kuwaza kama angekaa awe Rais.
Sijui kama unauona ugumu huu.! Imagine Mungu anakuahidi utakua "first
lady", halafu anakataa usichumbiwe na Mbunge. Anakupa mchumba mwingine,
halafu huyo mchumba anakwambia "sina hata ndoto za Urais". Ingekua ni
wewe ungejisikiaje? Wengine mngemlaumu Mungu na kutamani kurudi kwa mbunge,
right? Lakini Mungu akiahidi ni lazima atimize.
#Lesson_5: Mungu huinua vyenye nguvu katikati ya vinyonge.
Unakumbuka hadithi ya Daudi? Yesse alipoambiwa aite watoto wake wote maana
mmoja wao atakua Mfalme, aliita wote akamsahau Daudi. Imagine baba yako mzazi
anakusahau. Lakini Mungu akamfanya huyohuyo mdogo, mnyonge, aliyesahaulika kuwa
Mfalme. Lincoln nae pengine alionekana mnyonge, lakini Mungu akasema "huyu
ndiye"
Katika maisha usimdharau mtu yoyote. Heshimu kila mmoja.
Unayemdharau leo aweza kuinuliwa kesho ukabaki unashangaa. Ipo nguvu
iliyofichwa (the hidden power) kwa kila mmoja wetu. Unaweza usiione nguvu hiyo
leo lakini ipo siku itafanya kazi.
The secret behind hidden power.!!!
Comments