Popular posts from this blog
Taarifa za msiba...
By
inno.mosha@gmail.com
-
Kwa masikitiko makubwa nawataarifu msiba mkubwa tulionao leo. Ndugu yetu, mpendwa wetu, mwenzetu kwenye TEKNOHAMA na mdau mkubwa wa tafiti mbali mbali za TEKNOHAMA Kaka Andrew dACHI amefariki leo asubuhi nyumbani kwake Fransic Town, Botswana. Kwa sasa sina la ziada, ila tutaendelea kupeana taarifa kadri zitakavyotufikia. Tunaungana na familia yake, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo, kumwomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi, wakati taratibu za mazishi zinafanyika. Bwana alitoa, nae ametwaa. Jina lake lihimidiwe. tunaweza kujikumbusha moja ya kazi zake kwa kufungua ' http://www.isaconsulting.biz /' email yake ilikuwa ' andrew.dachi@isaconsulting.biz '
HARUSI YA KAKA YETU ND. MOSES MUDONKO...
By
bongotambarare
-
Bwana Harusi Moses Mudonko na Mkewe wakipongezwa na Joe Mnzavas siku ya harusi yao. Harusi hii ilifungwa kanisa katoliki na baadae kwenye tafrija ya kukata na greda pale Belinda Beach Hotel. Yasini Kilima (Mwenye shati la batiki), akifuatiwa na Nehemia Mwenisongole na wageni waalikwa wengine kumpongeza bwana harusi Moses Mudonko na mkewe. Maharusi pamoja na wapambe wao wakipongezwa na wadau mbali mbali pamoja na wake zao, kasoro Nassoro Siriwa ( wa kwanza kushoto, mwenye shati jeupe na tai) na almaarufu braza Carlos (wa kwanza kulia mwenye suti ya nguvu ya rangi ta brauni nyepesi) wadau hawa sijui kwanini hawakutokea na wapendwa wao? BLOGU HII KWA NIABA YA WADAU WAKE NA MIMI MWENYEWE NAWAPA MAHARUSI PONGEZI ZA NGUVU NA KUWAOMBEA KWA MUNGU, AWABARIKI NA WABARIKIWE SANA. HONGERENI SANA . KICHWANGUMU.
Comments