Tanzania nakupenda...

TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE
1. Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuwaza wewe, niamkapo ni heri mama wee

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.
2. Tanzania Tanzania, ninapokwenda safarini,
Kutazama maajabu, biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu hakika

Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.
3. Tanzania Tanzania, watu wengi wanakusifu,
Siasa yako na desturi, ilituletea uhuru
Hatuwezi kusahau sisi, mambo mema ya kwetu hakika
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.


Swali,

Je leo hii tunaweza kusimama na kuimba wimbo huu, tukiwa kifua mbele na furaha
kama enzi zile? nahisi umaarufu wa wimbo huu umepotea, hata mashuleni sidhan kama
unaimbwa tena, au na wenyewe ulikuwa ndani ya kale kakitabu ka AZIMIO LA ARUSHA.

Naomba kuwakilisha...

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.