Gari la pesa ladondosha pesa.

 
Polisi wa jimbo la Ohio, nchini Marekani wameuambia umma kwamba makumi ya maelfu ya dolari za Kimarekani yametoweka siku moja baada ya begi la fedha kuanguka toka katika gari maalumu la kusafirishia fedha. Inasemekana begi hilo lilipasuka baada ya kuanguka na niti za dolari 20 kuanza kupeperuka hovyo.

Raia baada ya kuona urali unapeperuka hovyo wakaanza kuacha shughuli zao na kuanza kujikusanyia kwa kadri walivyoweza. Hadi asa hakuna uhakika ni kiasi gani haswa kimetoweka japo vyombo vya habari vya Marekani vinakisia kuwa ni karibu dolari 100,000 za Kimarekani.

Polisi wa jimbo la Ohio wako katika msako mkali wakitumia kamera za video za ulinzi pamoja na picha za video zilizopigwa kwa kutumia simu za mkononi za baadhi ya watu waliokuwamo katika eneo la tukio. Sajenti mmoja wa polisi alisikika akisema, "Hizi zi fedha za bure".

Iwapo watu watakamatwa na fedha zinazoaminika kuwa ni zile za eneo a tukio watashtakiwa, anasema Sajenti Dan Kelso alipokuwa akizungumza na shirika la habari la AP. Anasema hana uhakika ni kwa vipi fuko hilo lenye neema lukuki liliweza kuporonyoka katika gari hilo maalum la kusafirishia fedha.

Mmoja wa watu alishuhudia tukio hilo live alisema aliona watu wakiacha magari, baiskeli, pikipiki, na hata kazi zao ili kujikusanyia fedha hizo zilizokuwa zinapeperuka huku na huko. Anasema hii ilikuwa ni siku ya neema kwa watu wengi hasa ukizingatia kwamba watu wengi sasa hivi wamepigika kupita kiasi kutokana na msoto wa uchumi mbovu duniani.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.