HESHIMA KWA WANAWAKE WOTE!!!!

Kuna tukio nililiona MAISHANI:Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote;HEBU IMAGINE:

ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau!!!

UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!

UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGIZZ: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.

UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!

CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!

UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!

UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!

Na mengineyo meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE,WANAVUMILIA, NA WANASAHAU! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!

HIVI INGEKEWA WANAUME TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?

Kwa leo acheni tu niwape heshima zao wanawake wote:

I SALUTE AND LOVE THEM WOMEN!
 
Mdau kutoka ISSA MICHUZI BLOG

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.