Kuwa meneja bora wa ICT


Kipindi nipo chuo kikuu nimewahi kushiriki au kuongoza project mbalimbali za IT na zisizo za IT,kuna baadhi ya project hakuna mtu aliyewahi kudhani kuwa inaweza kufanikiwa,hii ni kutokana na ugumu wake.

Kwa kipindi hicho chote nimekuwa nikipata mafunzo mengi ya jinsi gani ya kuwa manager mzuri sio tu wa IT bali hata nyanza nyingine mbalimbali.Kitu kikubwa sana nilichojifunza ni jinsi gani ya kuchagua watu husika(right people) kwa project husika,jinsi ya kumaliza kazi kwa wakati ndani ya bajeti nk.Kuwa manager mzuri mara nyingi inategemea sana ni jinsi gani unavyoshirikiana na wana member wako.

Kitu kikubwa nilichojifunza nikiwa China ni kuwa bosi ataendelea kuwa bosi na mfanyakazi ataendelea kuwa mfanyakazi ila kati yao mahusiano ni mazuri mno,bosi hana kujidai au kudharau walio chini yake,ukiwa nje ya ofisi ya bosi kuna kipindi unaweza usijue nani ni bosi,hawana yale mambo ya mimi ni bosi bwana.Hii inasaidia sana na kuongeza malali wa wafanyakazi.Hivyo basi leo hii nitakupa mambo machache tu ya jinsi gani unaweza kuwa IT manager mzuri.
1: Sikiliza wafanyakazi wako
Kitu cha msingi sana ni kuwasilikiza wafanyakazi wako,pata ushauri toka kwao na ufanyie kazi iwezekanavyo.Kwani wao ndio wanaojua hali halisi ya kampuni au project husika.Kuna kipindi niliwahi kuchukua project moja nzito,binafsi nikafungua milango kwa wafanyakazi wote kutoa maoni muda wowote,nikaondoa ukingo kati yangu na wafanyakazi,hivyo nilikuwa napata mawazo mengi mno na tulifanikiwa kuwashinda wapinzani wetu na kuwaacha wakibaki midomo wazi.Epukana na uongozi wa kizamani wa kusema mimi ni bosi bwana,hii iytakufanya utengeneze uhasama na kuondoa molali wa utendaji kazi kwa wafanyakazi wako. Jamani kumbuka kuwa sio lazima ufuate kila ushauri unaopewa,ila kuwa tarayi kupokea ushauri halafu ufanyie kazi.
Kitendo cha kuwasiliza wafanyakazi wako kitakusaidia kuwajengea moyo kuwa mchango wetu unathaminika ndani ya kampuni.


2: Kuwa mwerevu
Kitu kingine nilichojifunza kama IT manager ni kuwa msikivu,project nyingi za IT huwa zinachukua muda mrefu mno,muda mwingi inalazimika hata kupitisha muda wa kazi,chukulia mfano muanadevelop programu fulani na ghafla kunatokea matatizo kibao,hali kama hii ni kitu cha kawaida kwenye ulimwengu wa IT,hivyo basi unatakiwa kufikiria katika uhalisia wake.Kwa mfano kuna kipindi munatakiwa kufanya kazi zaidi ya muda ila akaja mfanyakazi na kuomba ruhusa anakwenda kupokea mtoto toka shuleni.Kama IT manager lazima uwe mwerevu wa jinsi ya kusikiliza maombi mbalimbali.Hii itasaidia kuongeza ufanisi wa kazi.Ila kumbuka lazima uwe mpambanuaji ili kupunguza mategeo.


3: Endeleza ufahamu wako
Kama tumeona mara nyingi maCIO au mameneja wengi hutumia muda mwingi mno kwenye vikao na semina mbalimbali,hii huwafanya kusahau au kutupilia mbali kabisa fani zao au ufahamu wao kiteknolojia(IT).Hawana tena muda wa kuconfigure server au kutatua matatizo ya kiufundi hii huwapelekea kupoteza maarifa ya kiufundi.Kuna sababu zinazoweza kukupelekea wewe kufaidika kutokana na kujiendeleza kiufundi hata kama wewe ndio manager.


Moja:Usiwape picha wafanyakazi wako wafikirie kuwa wewe hakuna kitu,hii inaweza kupelekea kukudharau au kukuongopea.Kumbuka kama hunaelimu ya kutosha ya IT halafu ukawa IT manager wa IT,wafanyakazi wako ni nadra sana kukuheshimu,hapa simaanishi kuwa ni lazima uwe geek,inatakiwa kujua mambo ya msingi tu.Mabosi wengi wa nchi zetu zinazoendelea wanakabiliwa na hili.Mfano mzuri tu,angalia mavyuoni,kama Mhadhiri anajiamini na mwenye ufahamu wa kutosha,ni nadra sana kuona anawakamata watu kwenye mitihani au kutopendwa na wanafunzi,ila wale wenzangu na mimi huwa na tabia ya kuwakamata watu kwenye mitihani ili kujenga uoga kitu kitakachopelekea wanafunzi kujenga uoga na kutomshambulia au kumuliza maswali ya kiufundi zaidi.

Pili:Nani anayejua nini kitatokea muda gani,inawezekana mupo katikati ya project halafu mfanyakazi mmojawapo akaugua au kusafiri,je mutaahirisha project kipindi munasubiria mtu mwingine kuajiriwa? Kama una ufahamu kidogo unaweza kushikiria kwa muda fulani kipindi muaendelea na kazi,Hii imewahi kunitokea,tulikuwa na project moja halafu baadhi ya washiriki wakajitoa,kutokana na ukweli kuwa nilikuwa na uwezo wa kufanya kama alichokuwa anafanya mfanyakazi aliyejitoa hakunaathari iliyotokea,nilichukua nafasi kipindi tunaangalia mtu mwingine wa kumuajiri.Hii sio tu kwenye mambo ya IT bali project zote.


4: Jua wapi pa kupata msaada wa ziada
Ukweli unabaki palepale hakuna anayejua kila kitu kwenye uwanja wa IT. Unapokuwa kama maneja kumbuka kuwa kila mfanyakazi ana anachokijua kwa undani na kuna asivyovijua kabisaa. Kuna kipindi unaweza kupokea project ambayo hakuna mfanyakazi wako mwenye uwezo wa kuifanya,kwa wale wenye uzoefu hapa watajua nini ninamaanisha,vijana wa siku hizi tunasema hakuna kuacha project,ipokee halafu utaangalie mbele kwa mbele. kama IT manager hautakiwi kuogopa kuipokea project eti kwa sababu wafanyakazi wako hawana uwezo wa kuifanikisha.


5: Pata mapumziko ya kutosha
Ukweli usiopingika ni kuwa kazi za IT ni mojawapo ya kazi zinazochosha na kutumia ubongo mno, kipindi tunamalizia project ya AfroIT kuna kipindi tulikwa tunalala kwa masaa mawili hadi matatu,ukiamka unakutana na makosa kibao huku kalenda ikionesha kuwa muda umekwisha. Nikiwa kama CO kuna siku kadhaa sikulala kabisa,huwezi amini. Hivyo basi ukiwa kama IT manager inatakiwa kutafuta muda wa kupumzika na kuondokana na uchovu na msongo wa mawazo. Bila ya hivyo unaweza kujikuta unakimbia barabarani, au kukufanya kupoteza mahusiano mazuri kati yako na wafanyakazi,je haukuwahi kuona ni mara ngapi bosi amekuwa akifoka kila kitu? Hii ni kutokana na misongo ya mawazo,kitu kitakachopelekea kupunguza ufanisi wa kazi.

Habari kwa hisani ya michuzipost na JamiiForum

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.