LIBYA... Sioni Mbele!

Nawasikitikia sana wananchi wa Libya kwa kuingia kichwa kichwa kwenye mkenge wa ukoloni mambo leo. 

Sasa tusubiri kuona wababe wa vita wakigawana Libya kama Somalia! Na sijui kama itatokea Libya kuwa na amani tena... Ukizingatia kwamba kama taifa moja la Afrika halina amani, utulivu kwa Afrika ni ndoto na ukoloni mambo leo ndio unazidi kupamba moto! Afrika haitakuja kuwa na maendeleo! Maskini Gaddafi...

Wa-Libya watajuta maisha... ndio imetoka hiyo! Inasikitisha sana! KICHWANGUMU.

Comments

Papaa said…
Kwa kweli ni maneno ya kweli na yenye kutia uchungu... ukikumbuka kuwa huyu Gaddaf ndiye aliyekuwa na ndoto ya kuunganisha Africa. kungekuwa na marais wengine watatu tu asingeng'oka...

Vibaraka wako wengi... hii nayokuwa ni kweli watanzania waliokuwa wanaishi pale Tripol wanasema kuwa wanawaona wake wa marais wa africa wakienda kukinga makopo yao pale kwa Gaddaf leo wote hawako wako kimya....

Nadhani Gaddaf anawashangaa akijua yupo na wenzake kumbi njaa tu leo huna wanakukimbia.

Papaa
bongotambarare said…
Papaa, ni kweli kabisa. Kwa mtazamo wangu, kilichosababisha wababe kumtoa gaddafi ni viwili vifuatavyo:-

1. Wazo lake na nia yake ya kutaka kuunganisha Africa yote! ili tuuziane ndani kwa ndani, na soko tunalo. tukiuza nje ya Africa tunapeleka 'finished products' sio 'raw material'. Hii ingewamaliza kabisa hawa jamaa.

2. Nia yake na wazo lake la kusisitiza kupandisha bei ya mafuta kupitia OPEC na kutaka itumike dhahabu kununulia mafuta badala ya 'dola' iliyokuwa ikiporomoka kinoma.

Haya mawili ndio chanzo cha dhuluma yote hii anayofanyiwa Gaddafi. Maana kama ni kubadilisha madaraka tumeona Kenya, Zimbabwe, nk. Mbona haikuwa vita? iweje Libya!?!?!?! Tena wanashiriki NATO! Walibya wanasikitisha sana, upeo wao sijui vipi hawa?

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.