Mnadani, Singida...

 Jana nilibahatika kutembelea moja ya minada ya Jumamosi mkoani Singida. Mnada huu upo njia panda ya Arusha na Dodoma ukitokea Down Town Singida. Picha ya juu inaonyesha barabara hiyoooo... Nachukua nafasi hii kuipongeza serikali yetu kwa dhati kabisa kwa juhudi kubwa za kuboresha miundombinu ya barabara. Kwa sasa kutoka Dodoma mpaka Singida ni lami tupu, kutoka Singida mpaka Arusha napo lami tupo. Mambo safi, ingawa bado zipo changamoto nyingine, ila kwa pamoja tutafika...
 Njiani pande zote mbili za barabara kuna vyanzo vingi vya upepo unaoweza kutumika kutengenezea umeme. Kama picha ya juu na chini vinavyojionyesha. juu ya hivyo vilima vidogo vya mawe kuna upepo mkali sana.

 Hapa tumeshaingia mnadani, tunapata nyama kiasi ya kuchoma, kwa walaji wa nyama watanielewa nikisema ilikuwa inavutia balaa! Frank Brown upo?
 Pichani juu na chini unaona nyama zilivyo nyingi. Hapa mnadani inaonyesha ni pahala maarufu kwa wakazi wa Singida kujumuika kila Jumamosi, pia wenyeji hunufaika na mnada huu kwa kuuza mifugo, mazao, vinywaji na huduma za kuchoma nyama, nilibahatika kukutana na watu ambao sikutegemea kuwaona.

 Hapa tulivutiwa na nundu ya ng'ombe kama uionavyo kwa pembeni kushoto kabisa! inavutoa... lol!
 Unaweza kuona mbuzi nao walivyo wengi... nilijiuliza "watakwisha kweli hawa?" wenyeji wangu wakaniambia wanaisha! kwa kweli kuna biashara...
 Nundu ya ng'ombe kwa karibu... ikichomwa hii... wacha kabisa!
 Pilika pilika za kuchoma zikiendelea, juu na chini...

 wadau mbali mbali wakiwa mnadani...
 mpaka majiko ya kisasa ya kuchoma nyama yapo mnadani kama pichani juu unavyoona. Picha ya chini ni ile nyama tuliyonunua pamoja na nundu ikiwa jikoni.

 Nundu iliiva mapema ikaja mezani... kama uionavyo!
 ikafuatiwa na nyama... kama uonavyo juu na chini. Nyama ilikuja kwa awamu, zilikuwepo awamu tatu.

 uchomaji wa nyama ukiendelea. hadi utumbo unachomwa... kama uonavyo katikati ya jiko.
 Kama nilivyodokeza awali, changamoto ni nyingi. hapa wadau wakienda kijisaidia kwa pembeni kidogo ya mnada. Hakuna vyoo... Bwana Afya wa Mkoa, changamoto yako hii! Kwa mbali, unaona mlima, chini ya mlima huo kuna bonde la ufa...
 Pichani juu na chini watu wakijisaidia... hii ni changamoto muhimu kuikabili ili kuweka hali ya usafi na usalama wa afya za wakazi na wageni wa Singida wanaohudhuria minada hii. Biashara ni kubwa kwenye hii minada, ni jukumu la Halmashauri kuweka miundombinu ya usafi. Sipendi kushauri ubinafsishaji wa hii miundombinu ya mnadani. Ni imani yangu kwamba Halmashauri kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa wanaweza kulishughulikia hili.
Kwa ujumla nilifurahi sana, ila nasisitiza usafi, uwepo wa vyoo, maji safi ya kuoshea nyama, na mikono ya walaji, na miundombinu mingine ya mnadani. Nia ni kuboresha na kuongeza biashara, hatimaye kodi nayo itaongezeka.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.