Today's Joke...


Ticha mgeni wa somo la historia wa darasa la saba, aliamua kuwachemsha wanafunzi wake kabla ya kuanza kipindi.

Akawauliza,"ni nani aliyemuua Mkwawa"?
Wanafunzi kimyaaa! Akaamua kuchagua wa kujibu.

Denti wa 1: Sio mimi mwalimu,hakyaMungu.
Denti wa 2: Kweli ticha sikumuua mkwawa,hata simfahamu kwanza
Denti wa 3: Mwalimu sio mimi,kwanza jana sikuja shule.

Mwalimu akaona hapa hana darasa bali kundi la majuha.
Akaenda kwa mwalimu mkuu kumwambia. Ticha mkuu akaenda kwa hasira ktk lile darasa na kuuliza lile swali,majibu yakawa yale yale,kila mtu "sio mimi". 

Mkuu kuona vile,akamvuta yule mwalimu pembeni na kumuuliza,
"una uhakika lakini kwamba huyo muuaji aliyemuua huyo mkwawa yupo humu ndani? Isiwe unanipotezea tu muda. Kama vp tukaite polisi"

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.