Eric na ndugu zake wapata ajali...

 Ilikuwa ni siku ya ijumaa tarehee 9 saa 12.30 asubuhi nilipokuwa nasafiri kwenda tanga kumzika bibi yetu mkubwa kupitia njia ya bagamoyo. Kilomita moja kabla ya msata. Gari linaloonekana kwa karibu ndilo lililonivaa na kupasuka engine hapo hapo. Gari nyeusi porini ndo gari nililochomoka humo na tulikuwa ndugu wannne. Peke yangu ndo nilitoka bila jeraha. Mmoja alivunjika mguu wa kulia, mwingine nyonga ilishtuka, na mwamnamke mmoja aliumia kizazi, aliyevunjika katoka hospitali jana (12th March 2013), na wote bado wapo nyumbani. Mdau Erick

Kwa niaba ya Kichwangumu blog na mimi mwenyewe, nawapa pole kwa ajali na maumivu. Pia, nawasihi waathirika wote tumshukuru Mungu kwa sababu hakuna aliyepoteza maisha. Poleni sana mdau Eric na ndugu zake.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.