R. I. P. Jovin Shumbusho

Jovin Shumbusho enzi za uhai wake.
Ndugu Jovin Shumbusho (pichani), aliyekuwa Principal Tax Investigations Oficer wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Upelelezi wa Kodi, Amefariki dunia jana jioni katika hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha "ICU". 

Jovin Shumbusho alisumbuliwa na uvimbe kwenye ubongo, uliopelekea aende nchini India kwa matibabu na kufanyiwa upasuaji. Alirudi Tanzania na kuendelea na dawa pamoja na uangalizi wa madaktari kwa muda wote.

Mipango ya mazishi tunasubiri taarifa rasmi kutoka kwa familia yake. Msiba upo nyumbani kwake Makongo Juu, Dar es Salaam. Tulimpenda sana Kaka yetu, Mshauri wetu, Kiongozi wetu, Mume kwa mkewe Eva, Baba kwa wanae Nancy na Jovin Junior, Mtoto kwa baba yake Mzee Shumbusho, lakini Mungu amempenda zaidi. Utukufu Juu kwa Mungu milele amina.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe. Mungu Baba Mwenyezi aiweke roho ya Kaka Jovin Shumbusho mahala pema peponi. Amen.

Kwa niaba yangu binafsi na familia yangu na wana jamii wote wa blogu hii, tunatoa pole za dhati kwa familia ya Hayati Jovin Shumbusho na kuwaombea rehema za Mungu, uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu. Siku zote tunaamini Mungu ni mwema na tunashukuru kwa kila jambo. Sifa na Utukufu ni kwake Mungu Baba Mwenyezi. Amen.

Tutazidi kuwataarifu taratibu zote na mipango ya mazishi kadri tutakavyoipata.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.