FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016



Nembo ya Shirika la Kimisionari la Bikira Maria Mama wa Yatima. Niliikuta nembo hii nilipoingia nyumba ya Masista wa Shirika hili kwenda kumwona Sista Restuta. Hapa nilipelekwa na Pius baada ya kupata ruhusa ya Mlinzi.
Sista Restuta (Mama wa watoto hao) akiwaandaa wanae kuimba nyimbo kituoni hapo.



 Chakula kilichoandaliwa na familia yangu kwa ajili ya watoto hao
 Sehemu ya kukaa wageni na watoto wa kituo cha Furaha Mbweni Kijijini.
 Watoto wakichukua chakula. Sister Restuta na utawala wa kituo umeweka utaratibu mzuri sana wakati wa kula. Wanaanza watoto wa Chekechea (Nursery School), wakifuatia wa Shule ya Msingi kuanzia darasa la Kwanza kuendelea mpaka Kidato cha Sita. Kituo hiki kunachukua watoto wa kuanzia miaka mitatu ambao wanasoma Chekechea
 Watoto wakiendelea kuchukua chakula
 Huyu mtoto wa kushoto mwenye fulana nyeupe anaitwa Pius. Alinipokea siku moja kabla nilipokwenda kupeleka vyakula vyao na kufanya maandalizi ya siku hii rasmi. Alinipeleka mpaka nyumba ya Masista ambapo nilikutana na Sista Restuta kwa mara ya kwanza. Hatimaye nasisi urafiki wetu ukaanza.
 Mwanangu Ivanna akiwa na dada yake Julie wakipata chakula cha mchana. Ivanna ndiye mwenye msukumo wa kuwatembelea watoto yatima. Amekuwa akinisisitiza tangu nilipompa ahadi hiyo Mwezi wa Disemba Mwaka 2015 alipokuwa likizo. Akiwa Chekechea ya Mtakatifu Josephine Bhakita alikuwa anatoa sadaka maalum ya yatima kila siku ya Ijumaa. Namshukuru Mungu kwa ukarimu wake. Mungu azidi kumlinda, kumsimamia na kumariki akue hivyo hivyo.
 Dada yangu Anna akiwa na mwanae Junior wakipata chakula.
 Dada yangu mwingine Pili akimlisha Alfred 'Kipoo' Junior.






 Julie, Ivanna na wadogo zao wakikabidhi vifaa vya Shule (Madaftari, kalamu, nk) kwa watoto wazuri wa Kituo cha Watoto Yatima cha Furaha Mbweni.



Julie akipokea baraka kutoka kwa Sista Restuta huku Ivanna akimwangalia.

Kituo hiki cha Furaha kipo Mbweni Kijijini nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kinasimamiwa na Masista wa Katoliki wa Shirika la Kimisionari la Bikira Maria Mama wa Yatima. Mimi na familia yangu tunamshukuru sana Mungu kwa kupata wazo la kutembelea na kupeleka vifaa vya shuleni (Stationeries) pamoja na chakula, pia kuweza kuandaa chakula cha Mchana.

Kuwa na nia au wazo ni suala moja lakini kupata baraka za kutekeleza wazo hilo ni suala lingine. Naamini ni kwa uwezo wake Mungu Pekee ndio tumefanikiwa. Nawasihi na kutoa wito kwa watu wengine wote tuwe na moyo wa kuwasaidia na kushirikiana na Watoto hawa Yatima. 

Watoto Yatima ni wetu sote. Masista hawa wanafanya kazi kubwa ya kuwalea Kiroho, Kielimu na Kimwili. Sisi wengine ambao Mungu ametujalia maisha, afya njema na nguvu hatuna budi kuwaunga mkono na chochote kidogo tulichonacho ambacho tupo tayari kushirikiana nao.

Natoa shukrani zangu za pekee wa watumishi wote wa Kituo hicho hasa Sista Augusta ambaye alinipokea siku ya kwanza nilipokwenda kujua utaratibu wa kutoa zawadi. Pia, namshukuru Sista Restuta kwa ushirikiano mkubwa alionipa mimi na familia yangu tangu siku napeleka vyakula na kuchukua bajeti ya kuandaa chakula cha siku hii. Nawashukuru pia walinzi kuanzia Dada Neema Mremi na wengine wote.


Ahksanteni sana. KICHWANGUMU.

Comments

Kishimba said…
Safi sana Bro, nimependa sana hilo tukio. Nawaombea wewe na familia yako muendelee kuwa na moyo wa aina hiyo siku zenu zote. Pia my special thanks to Ivana...its a very nice spiritual life for her and at her age...bravo Mr. & Mrs. Inno Mosha kwa malezi mazuri ya kiroho. Mwisho nanyi mtuombee nasi wengine tuweze kuiga na kufuata mfano wenu.

Kishimba!
Unknown said…
Mungu awabariki sana. Tutawatembelea hawa watoto mwanzoni mwa mwezi ujao, Novemba.

Popular posts from this blog

Taarifa za msiba...