Kamilioni aanguka na kuvunjika Arusha

MSANII maarufu wa Uganda, Jose Chameleon amejirusha kutoka ghorofa ya tatu ya Hoteli
ya Impala mjini Arusha na kusababisha kuumia vibaya ikiwa ni pamoja na kuvunjika
miguu yote.

Chameleon ambaye amekuwa akitamba na nyimbo za ‘Jamila’, ‘Mama Mia’ na
nyingine alijirusha kutoka chumbani kwake katika ghorofa ya tatu ya hoteli hiyo
alfajiri ya saa 11 kuamkia juzi.

Imeelezwa msanii huyo alishituka akiwa chini amevunjika miguu hiyo na walinzi
walikimbilia eneo aliloangukia baada ya kusikia kishindo na kumkuta akiwa hawezi
kuinuka.

Hata hivyo haikueleweka kilichomfanya msanii huyo ajirushe, baadaye wenyeji wake
ambao ni Clouds FM waliokuwa wamemualika kwa ajili ya shughuli ya Fiesta ya Tanga
juzi walibidi kufanya utaratibu wa kumpeleka hospitali.

Lakini baadaye walitakiwa kutomtibu na baba yake aliagiza ndege ambayo ilitua kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA na kumbeba na kumpeleka Uganda ambako amelazwa
katika hospitali moja ya nchini humo akipata matibabu.

Kuumia kwa msanii huyo kulisababisha ashindwe kufanya shoo katika tamasha la Fiesta
ambako kulikuwa na wasanii wengi wa Tanzania na yeye ndiye alikuwa mgeni aliyetakiwa
kuongoza shoo hiyo.

Source: JamiiForum

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.