Kinywaji cha Red Bull- Cola chapigwa marufuku Tanzania


================================================================================
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini [TFDA] imepiga marufuku uingizwaji wa kinywaji cha Red Bull-Cola nchini ikieleza kuwa hatari kwa afya za binadamu kwa kuwa ina asili ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Gaudensia Simwanza ofisini kwake jana.

Amesema mamlaka hiyo kwa sasa inaendesha msako mkali nchini kubaini watu wanaoagiza kinywaji hicho ambacho kimeshakatazwa kuingia nchini kwa sababu hizo.

Alisema Mei mwaka huu walipata taarifa kwamba kinywaji hicho ni hatari na moja kwa moja mamlaka ilianza kujipanga kukidhibiti kuingia nchini.

Simwanza aliwataka wananchi kuwa makini na kinywaji hicho mana wanatangaza kupitia vyombo vya habari ili wapate kuelewa, na watoe taarifa pindi wanapokuta kuna mahala wanauza kinywaji hicho hatarishi ya afya.

Pia alisema na kufafanua kuwa kinywaji cha Red Bull (original sio Redbull cola) kinachouzwa Tanzania hakina kilevi cha aina yoyote na kwamba hakina madhara kwa matumizi ya binadamu ila aina hiyo ya Cola ndiyo ina madhara na kuwataka watanzania wawe makini wanapotumia kinywaji hicho kutazama aina.

Alisema kuna ongezeko kubwa la uingizaji wa dawa na bidhaa kupitia njia za panya, ambapo udhibiti wake umekuwa mgumu na kusababisha bidhaa feki kuingia sokoni bila kibali cha Mamlaka hiyo.

Alisema kuwa mamlaka hiyo ndani ya miezi mitatu imekataza matumizi ya maziwa ya watoto wachanga mara mbili ambapo awali ilikataza maziwa kutoka China aina ya Nido yaliyokuwa na kemikali aina ya melamine na hivi karibuni wamegundua kuwa maziwa aina ya S26 kutoa Afrika ya kusini yana vimelea vya magonjwa.

Na tayari wameshateketeza tani zipatazo 30 za maziwa ya watoto yaliyopigwa marufuku hivyo watanzania wanatakiwa kuwa makini sana kwa kulinda afya zao na za watoto wao.

Mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi nchini hasa kwa kipindi cha hivi karibuni cha kuibuka kwa wimbi la uingizwaji wea madawa ya kuongeza maumbile kwa akina dada na tayari watu kadhaa wameshafikishwa mahakamani kwa makosa ya kukutwa wakiuza madawa hayo.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.