Mtoto wa Mwaka Mmoja Mwenye Mimba Awashangaza Madaktari China




Madaktari nchini China walipigwa na butwaa baada ya kugundua kuwa mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja ambaye alipelekwa hospitali baada ya tumbo lake kuzidi kuwa kubwa, alikuwa na mimba ya kichanga kingine. Picha za mtoto huyo mwisho wa habari hii.

Mtoto Kang Mengru wa nchini China alipelekwa hospitali baada ya wazazi wake kushtushwa na hali ya tumbo lake kuzidi kuwa kubwa siku hadi siku.

Baada ya mtoto huyo kufanyiwa ultrasound, madaktari waligundua kuwa mtoto huyo wa kike alikuwa amebeba kitoto kichanga kwenye tumbo lake ambacho kilikuwa kikiendelea kukua.

Madaktari wanaamini kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa na mimba ya watoto wawili mapacha na pacha mmoja alijitokeza ndani ya tumbo la pacha mwenzake.

Hali kama hiyo ya kichanga kuzaliwa ndani ya kichanga kingine ni nadra sana kutokea na humtokea mwanamke mmoja katika wanawake 500,000.

Mtoto Kang atafanyiwa upasuaji kukiondoa kichanga hicho tumboni mwake.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.