TFDA: Watanzania msitumie kondom za Hot

Na Shadrack Sagati

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imewashauri watanzania wasitumie kondomu ziitwazo Hot kwa kuwa haijathibitika kuwa ni salama kwa watumiaji.

Mamlaka za Kenya na Zambia zimepiga marufuku matumizi ya kondom hizo zinazodaiwa kutokuwa na ubora hivyo kuhatarisha usalama wa wanaozitumia.

TFDA imeamua kuanza kuzichunguza kondomu hizo zilizozua hofu kwa watumiaji baada ya kudaiwa kuwa zina matobo na kwamba, wananchi watafahamishwa matokeo ya uchunguzi huo.

Hot ni kondomu zinayotengenezwa nchini Uingereza.

“Tunawaomba watumiaji wa hizi kondomu waache kwa sasa wasubiri uchunguzi tunaofanya hadi tutakapojiridhisha ubora na usalama wa kondomu hizo,” amesema Afisa Uhusiano wa TFDA Gaudensia Simwanza.

Simwanza amesema leo kuwa,TFDA pia imeamua kuchunguza kondomu aina ya Contemto zinazotengenezwa nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Simwanza, miongoni mwa kondomu zilizoko kwenye aina hiyo ni Rough Rider na Durex.

Amesema, bidhaa zote zinazoingiwa nchini huwa zinafanyiwa uchunguzi kuona ubora na usalama wake, lakini pia kunaweza kuwa na toleo lenye matatizo.

“Kondomu kama vifaa tiba wakati mwingine kunaweza kuwa na toleo ambalo lina matatizo, hivyo ni jukumu la mamlaka kujiridhisha baada ya kuona baadhi ya nchi jirani zinagundua matatizo hayo,” amesema.

Simwanza amesema hafahamu uchunguzi huo wa kimaabara utakamilika lini kwa kuwa suala hilo ni la kitaalamu.

Mamlaka za Kenya na Zambia zimezuia uingizaji na matumizi ya kondomu za Hot baada ya kuzichunguza na kubaini kuwa zina matobo hivyo hazina ubora na usalama kwa watumiaji.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.