Nani mjinga????????

Kulikua na mabosi wawili wa kampuni moja ambao walikua wanapenda sana kutoka pamoja hasa siku za mapumziko. Walikua wanawatumia madereva wao kuwapeleka kila wanapoenda.
 
Kama ilivo kawaida kila bosi hujuana na dereva wake au boosi kumjua vilivyo dereva wake. Siku moja, jumapili, wakiwa wametoka na kuelekea maeneo ya ufukweni walianza kuzungumza na mazungumzo yakawa hivi:
 
Boss 1: aisee nakuambia sijawahi ona dereva mjinga kama huyu niliyenaye!
 
Boss 2: aaaaah we waongea nini……….huwezi amini huyo dereva niliyenaye yaani hamnazo kabisa.
 
Wakaendelea kubishana kila mmoja akisema dereva wake ni mjinga zaidi ndipo ikabidi wathibitishe kwa kila mmoja kuonyesha ujinga wa dereva wake.
 
Boss 1 akamuita dereva wake.
 
Boss 1: eeeeh chukua hii elfu 20 nenda kaninunulie TV dukani!
 
Dereva: sawa boss, vp niilete huku au niipeleke nyumbani?
 
Boss 1: ukiweza kununua ilete hapa.
 
Dereva akaondoka, boss 1 akasema: waona alivo mjinga yaani hata hajui kua kwa shilingi elfu 20 huwezi kupata TV.
 
Wakacheka, Boss 2 akasema sasa ngoja umuone dereva wangu alivyo mjinga.
 
Boss 2: hebu nenda nyumbani kaniangalie kama nipo!
 
Dereva: sawa bosi
 
Dereva akaondoka, Boss 2: waona alivyo mjinga, mimi nipo hapa alafu ataenda nyumbani kuniangalia kama nipo
 
Wakacheka na kusema kweli huyu mjinga.
 
Upande wa pili wale madereva wakakutana na kuanza kuongea.
 
Dereva 1: huwezi amini sijawahi fanya kazi na Boss mjinga kama huyu.
 
Dereva 2: bora wewe mi wangu ni punguani kabisa hata sijui kapata wapi ubosi.
 
Dereva 1: sasa sikia kaniita sahivi ananiambia niende nikamnunulie TV, wakati anajua fika kabisa kua leo ni jumapili na jioni hii hakuna duka lililowazi kama sio ujinga ni nini??
 
Wakacheka!
Dereva 2: hahaha aisee ila hata hivyo hafikii kwa upunguani wa bosi wangu, eti kaniita pale ananiambia niende nyumbani kwake nikamuangalie kama yupo, ilhali anasimu pale angeweza tu kupiga kwa mkewe nyumbani amuulize kama yupo au lah na sio kunisumbua mimi mpaka niende kwake!
 
Wakabaki wakicheka kila mmoja kuendelea na alichotumwa!
 
Je nani mjinga???? Mabosi au dereva??

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.