Cristians and Muslims join hands for their rights at Tahir square in Cairo, Egypt.

 Nani kasema unaweza kuwabagua watu kwa dini zao?!?!?!?! ammaaah! labda mazuzu... angalia hapo 'Tahir Square' Cairo, Egypt. Wakristu kwa Waislamu wote na vitabu vyao vitakatifu yaani Biblia na Quran. Tena kwa upendo wa dhati. Hii inatuthibitishia kwamba jamii iliyoishi pamoja kwa muda mrefu na kwa amani huwezi kuitenganisha kwa fitna za kidini. Labda kama haki haitatendeka na dini ikawa secondary reason.
Hapa inaonekana wakiweka uzio ili wenzao waweze kutimiza ibada. Inasemekana wakristu waliweka uzio Ijumaa ili wenzao waswali na waislamu waliweka uzio ili wenzao wasali Jumapili. Mshikamano dhahiri huo na funzo kwetu.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.