Vitimbi vya wazee...

Na Julius C. Lamosai, Morogoro.


Babu mmoja mzee sana alishinda bahati nasibu na kupata zawadi ya dola milioni 100. Waandaaji wa bahati nasibu hiyo wakaona wamshauri mjukuu wake ambaye ni daktari ili atafute njia ya kufaa ya kumwambia babu yake hiyo habari kwamba ameshinda maana waliogopa asije kupata mshtuko wa moyo. Basi yule mjukuu akaona amwanzie mbaali na akamwambia babu yake kwa upooole kama hivi;
Mjukuu: "Babu shikamoo”.
Babu: “Marahaba mjukuu wangu, karibu sana”.
Mjukuu: “Aksante babu. Dah, unakula kiporo cha wali asubuhi, kwanini babu?
Babu: “Ni shahuri ya maisha magumu mjukuu wangu, hela ya mkate hamna”.
Mjukuu: “Pole sana babu. Kwahiyo kwa mfano ukipata sasahivi dola za
     Marekani milioni 100 utafanya nini?"
Babu: “Na uzee wote huu...nitakupa wewe zote mjukuu wangu".

Yule mjukuu  akaanguka palepale kwa mshtuko wa moyo akafa!!!

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.