Hawa ndio wabishi wa karne!

Wapenda ligi watatu walibishana kuwa nani amekubuhu kwa ubishi kati yao . Wakaamua kila mmoja ahadithie ubishi wa haja alomfanyia mkewe ili wapime nani kubobea zaidi kwenye hiyo fani.

Mbishi 1 akasema:
Mi siku moja nilivyokuwa nje ya nchi nilimpigia mke wangu simu usiku kafungua simu hakusema haloo...kulaleki! na mimi nikakaa kimya sikuongea mpaka alfajiri wakati simu ilikuwa wazi.


Mbishi 2 akatia:
Mbona hiyo cha mtoto, mi siku moja nimerudi home nikagonga mlango mke wangu akaufungua lkn hakusema karibu mume wangu...aliniangalia tu...nikaona analeta madharau! sikuingia ndani nikasimama hapo hapo mlangoni mpaka asubuhi...huyoo nikatimua zangu job.


Mbishi 3 akaunganisha:
Hiyo nayo mbona cha mtoto tu, mi mke wangu tulipooana alikuwa anaona haya kunigusa...ananidengulia eti! na mimi sikumgusa na mpaka leo hatugusani.


Mbishi 1 na 2:
Aaaaaaaah faza! acha usanii, nyie si mna watoto wawili lkn?


Mbishi 3:
Na hao watoto sijamuuliza kawaokota wapi vile vile... kwani mi nataka mchezo!. Alaah...

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.