Nyama mabuchani zinapuliziwa Rungu!!! Take care...

Na Mwandishi wetu, DSM.

Uchunguzi wa kuaminika uliofanyika katika maduka mengi Dar, Moro na miji kadhaa mingine umegundua kuwa wauza nyama wamekuwa wakifanya mchezo hatari wa kupulizia nyama sumu za kuua wadudu ili kuzuia inzi. Sumu zinazotumika sana sana ambazo watu wengi hutumia kuua mbu ni rungu, Hatari, expel, Baygon, Hit, doom na nyinginezo.

Katika maduka mengi siku hizi ukienda utaona nyama imetundikwa sehemu ya wazi lakini hakuna inzi. Wafanyabiashara wa nyama wameona kuwa hiyo ndiyo mbinu ya kuvutia wateja ambao wengi hawapendi kununua nyama ambayo imekaliwa na inzi.

Uchunguzi huo ulifanyika kwa kuwauliza wauza nyama ambao baadhi walikiri kufanya hivyo ili kuvutia biashara. Uchunguzi pia umebaini kuwa pamoja na kufanya zoezi hilo kwa usiri mkubwa, baadhi ya wanunuzi wamekuwa makini kwa kuinusa nyama wanayonunua, kwani kwa kufanya hivyo harufu ya 'sumu' huwa dhahiri.

Napenda kuwatahadharisha tunapoenda kununua nyama tuwe makini, maana madawa haya japokuwa yanasemwa kuwa hayana madhara makubwa kwa binadamu, lakini mojawapo ya ingredient yake (piperonyl butoxide) iliyomo kwenye hizi sumu, inafahamika kuwa ina madhara makubwa kwenye kukua na kukomaa kwa ubongo hasa kwa watoto.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.