Ubishoo bila shule!!!!! NOMA...

Chekibobu mmoja aliyekuwa akijifanya anajua ung’eng’e huku akijifanya yeye ni matawi ya juu alikwenda kupata msosi yeye na demu wake.Si unajua mabishoo kwa kupenda kujikweza? Basi demu akaagiza chipsi kuku jamaa akaagiza wali nyama.

Baada ya kumaliza wakaletewa bili yao ambayo ilikuwa ni sh, elfu (15,000). Kumbe jamaa mfukoni alikuwa na kiasi hicho hicho cha pesa, akalipa lakini kwa shingo upande huku akimuomba Mungu yule demu asijekuagiza kitu kingine maana ataumbuka.

Ile wanainuka tu demu si akamuomba mhudumu amletee ‘tooth stick’ za kuchokonolea meno ambazo hutolewa bure kwa mteja. Yule brothermen kusikia vile akaanza kuwaka akijua kwamba atatakiwa kulipa wakati hana kitu mfukoni na kuwaka akisema “Sweet yaani unaagiza tena? Hizo ‘tooth stick’ utalipa mwenyewe” Demu kusikia vile akajua jamaa kumbe hakwenda hata darasa moja! Palepale kila mtu akashika njia yake...

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.