Tanzania Zinduka: Utapeli mpya kwa wamiliki wa nyumba Bongo...

Stori kutoka JamiiForum 

Nimekutana na habari kuwa upo utapeli wa aina yake ambao umeshawaliza watu wachache. Unahusiana na kundi linalokuja kwa lengo la kuja kupangisha nyumba na kufanya mambo lukuki hasa kwa watu wenye nyumba mpya. Mtu mmoja amesimulia hivi:

Quote:

Mmh ndugu zangu ni kwel hawa matapeli mimi mwenzenu nimeuvaa mkenge Morogoro na niliona ni wahitaji wa nyumba kweli na modus operandi waliyoitumia ni hiyo ya kuhonga TRA ILI MALIPO YAWAHI Wanatumia namba 0758409096 na 0682768889 ni vyema watu wa usalama waingilie kati asante kwa kunifumbua macho na masikio kwani nilikuwa naendelea kufanya nao mawasiliano
Na mwingine akadokeza

Quote:

jamani yamenikuta ni juzi walikuja kwenye eneo langu chanika ila sikufikia hatua ya kutoa hela walikuwa bado wapo kwenye mawasiliano na wakaniambia niende posta wamenitumia mkataba wa vitu wanayohitaji jamni tuweni mamcho mimi nashangaa kwa nini simu zimeshasajiliwa na hawakamatwi?nadhani kuna siri kubwa nadni ya mtandao huu..lakini siku moja watakamatwa tu.
Yaani ni jana tu ndio nimecheck mtandao nione ahiyo project ndio nakutana na watu wametoa comments zao kuwa wameshatapeliwa. Tuwemakini kwa kweli.
na mwingine akasimulia

Quote:

mimi niko amerika, najenga nyumba yangu hapo dar, fundi anayejenga nyumba amenipigia simu kuwa watu hao wa TANZANIA JAPAN ORPHON PROJECT WA SIMU NUMBER 0783-927-196 MR SABAI wana hitaji nyumba ya kupanga kwa miaka 2 kwa dola 800 jumla watatoa dola 19,200.00 kwa ajili wafanyakazi wao, wakasema watajenga fence ya umeme kuzunguka nyumba, kuchimba kisima cha maji, watamalizia kuweka umeme kama offer . Lakini baada ya kupata habari hiyo nikapiga simu kwenye ubalozi wa japan hapa USA wakasema hakuna shirika la namna hiyo na wakanitajia majina kama hayo uliyoolezesha kuwa ndiyo wamiliki wa shirika hilo haramu.OK WANAIBAJE? watakupeleka kwa wakili wao ambaye pia ni taperi mwenzao, unasaini mikataba mingi usiyoilewa na kwa vile mawazo yako yote yako kwenye lundo la pesa ya miaka miwili unasaini tu, lakini akili yao ni kukusainisha mkataba kwamba unawauzia nyumba kwao kwa bei hiyo ya kupanga kwa miaka miwili, sasa kwa vile wewe hujui baada ya miaka miwili ya mkataba wa kupanga kuisha ukiwambia ku-renewal mkataba watakucheka kwamba wewe uliwauzia nyumba, na ni kweli umesaini tena kwa wakali!!! kuweni macho sana.
Kama tulivyoifumua DECI lets stop do it again.. !!!
 
WADAU, KUWENI MAKINI... KICHWANGUMU.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.