Mazishi ya Marehemu George Mazula

Marehemu Capt George Mazula (aliyekuwa mkuu wa marubani wa ATCL wakati wa uhai wake) ataagwa rasmi kuanzia siku ya Jumanne usiku, nyumbani kwake mikocheni Dar es salaam. Jumatano asubuhi, mwili utaombewa kanisani (Jirani na nyumbani kwake) na baadae msafara utaelekea Leaders Club, ili kutoa nafasi kwa wana-jamii kutoa heshima zao za mwisho kabla ya mazishi katika makaburi ya Kinondoni, Dar es salaam. Alikuwa mgonjwa, akafanyiwa upasuaji wa mgongo nchini India, uliofanikiwa kwa kiwango kikubwa, akarudi nyumbani. Akiwa nyumbani alipata "attack" ya pumu, iliyomuumiza na kupelekea kifo chake.

Mungu ametoa, Mungu ametwaa, Jina lake lihimidiwe, Amen.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.