Kuwa makini na mitandao!!!!

Unapojiunga katika mitandao hiyo mingi huwa inatuma mialiko ( invitation ) kwenda katika anuani zako zote kama ni yahoo au gmail au hata hotmail bila idhini yako wewe , hii inaanisha kama mtu akipata mwaliko ule na kuwezi kujiunga atakuwa rafiki yako na ataweza kuona unawasiliana na wakina nani zaidi .

Wengine huwa wanaweka picha zao katika mitandao hii , mitandao hii haina sheria kali kuhusu picha zinazohifadhiwa mule hata kama ni za uwongo kama sio za matusi basi zinaachwa zikae hapo hapo , wengine huwa wanachukuwa picha katika tovuti hizo nakwenda kuzitumia katika maeneo mengine ya kazi zao au za kidhalilishaji zaidi

Mfano katika mtandao wa zeutamu kuna wanafunzi wengi sana wa IFM walikuwa wanapeleka picha kule ambapo zilitolewa facebook na hi5 au tagged wakaziedit kidogo kisha kuzituma zeutamu kwa faida zao wenyewe , wengi picha hizi wanazitumia katika magezeti na vijarida vyao bila idhini ya mfano facebook au hi5 hili ni suala la kisheria zaidi mimi sio mtaalamu wa sheria hata hivyo .

Kwa kuwa mitandao hii inavutia sana vijana wahalifu hutumia sana mitandao hii kwa ajili ya shuguli zao za kutafuta watu wa kuwasaidia kufanya uhalifu wao sehemu mbali mbali duniani , mfano unaona picha ya msichana mrembo sana katika mtandao , wewe unafikiria kuwasiliana nae ndio utawasiliana nae haswa walio nchi za mbali anaweza kukuomba umtumie pesa ili aweze kuja hapo ulipo wewe, ukishatuma pesa ndio unaweza usimwone tena na mawasiliano yakatike unakuta kuna watu zaidi ya alfu 2 wameona picha hiyo na wamependa kuwasiliana nae ( unaweza kuhisi anatengeneza pesa kiasi gani mtu huyo ?)

Wengine wanaona picha hizo haswa za wasichana walio katika nchi masikini wanawaahidi ajira nchi za ngambo wakienda kule ni kuuzwa kwenye madanguro pamoja na sehemu zingine za anasa utashangaa mbona ndugu yako harudi nyumbani wala hawasiliani kwanini ??

Hayo ndio mambo yaliyo katika mtandao jamii hii ingawa kuna wengine wanafanikiwa kufaidika sana na mitandao hii kwa kupata watu waaminifu wa kuwasiliana nao hata wengine kuowana na kufanya biashara ila wengi zaidi ndio wahanga wa matukio mengi ya kihalifu yanayoendeshwa kwa njia ya mtandao

Kwahiyo kijana mwenzangu unapotumia mitandao hii uwe makini sana kama hujui uliza upate uzoefu wa wenzako wanafanyaje kuweza kuhimili vishindo hivi vipya vya mitandao usiingie kichwa kichwa

Mwisho kama nilivyosema hapo juu mashirika mengi ya kijasusi na kipepelezi yanatumia mitandao hii kusaka wahalifu hata kutafuta wafanyakazi wapya basi hata hapa Tanzania vyombo vyetu vya usalama viwe makini sana katika kufuatilia mitandao hii pamoja na wanachama wake kwa faida zao na wengine

KICHWANGUMU!

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.