Kweli wazungu hamnazo!!!

Akodisha Mwanaume wa Kumbaka Mkewe!
Mwanaume mmoja wa nchini Marekani ametupwa rumande baada ya kumkodisha mwanaume aliyemtafuta kwenye internet ili ambake mke wake anayekaa naye ambaye amezaa naye watoto wawili. Polisi wa Marekani walisema kwamba mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 25 aliweka tangazo la kumtafuta mtu wa kumbaka mke wake kwenye interenet bila ya mke wake huyo kujua.

Mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa ili kuzuia kutambulika kwa mke wake, amefunguliwa kesi ya ubakaji na tuhuma zingine mbali mbali.

Mwanaume huyo mkazi wa Kannapolis katika jimbo la North Carolina alikuwa chumba kimoja na mkewe wakati mwanaume aliyemkodisha alipokuwa akimbaka mke wake.

Watoto wao wawili wadogo walikuwa nyumbani wakati huo lakini hawakujua chochote kilichokuwa kikiendelea chumbani kwa wazazi wao.

Baada ya tukio hilo mume huyo aliwapigia simu polisi akidai wamevamiwa na mke wake amebakwa.

Polisi waliyatilia mashaka maelezo yaliyotolewa na mume huyo kutokana na kwamba kulikuwa hakuna dalili yoyote ya mbakaji kuvunja au kutumia nguvu kuingia ndani ya nyumba hiyo.

Uchunguzi zaidi wa polisi ulipofanyika katika kumtafuta mbakaji ulifanikiwa kugundua tangazo lililowekwa kwenye internet na mume huyo akimtafuta mtu wa kumbaka mkewe.

Mke wa mwanaume huyo akiongea baada ya taarifa hiyo ya polisi, alisema kwamba alikuwa hajui chochote kama ubakaji huo ulikuwa umepangwa mumewe.

Haikujulikana mapema kama mbakaji alilipwa kiasi gani na mwanaume huyo ingawa inasemekana mume huyo aliamua kuchukua uamuzi huo ili kumfundisha adabu mkewe kwa kutumia vitisho.

Mwanaume huyo ametupwa rumande huku dhamana yake ikiwa ni dola 200,000.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.