Kasuku nae...

By Jovin Shumbusho
DSM

MWANAMKE mmoja alikwenda kwenye duka la wanyama na ndege akitaka kununua kasuku.

Cha kushangaza, akakuta kuna kasuku mmoja tu, mzuri sana ila bei yake ilikuwa ya kutupa, shilingi elfu moja tu. Ikabidi aulize mbona bei ndogo sana ?

Mwenye duka akamwambia kuwa kasuku huyo anauzwa kwa bei ndogo kwa sababu alikuwa anamilikiwa na changudoa na ana lugha za ajabu ajabu sana .

Kwa kuwa alivutiwa na kasuku huyo, ikabidi amnunue hivyo hivyo na kurudi naye nyumbani kwake ambako alimuweka sebuleni.

Alipomuweka tu, kasuku akasema, “Nyumba mpya, mwanamke mpya”

Nusu saa baadaye binti wa yule mwanamke akarejea toka shule, kasuku akasema, “Nyumba mpya, mmiliki mpya na binti mpya”

Jioni ilipofika baba mwenye nyumba, Mzee John akarejea toka kazini, kasuku akasema; “He! John, unafika mpaka huku!”

Comments

Popular posts from this blog

Taarifa za msiba...

HARUSI YA KAKA YETU ND. MOSES MUDONKO...