Shukrani

Kwa niaba ya familia ya Bw. na Bibi Kassidi wa Sinza, Dar es salaam. Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote walioshirikiana nasi kipindi cha msiba wa mtoto wetu mpendwa Arthur Francis Kassidi kilichotokea tarehe 23 Julai 2009 na kuzikwa siku hiyo hiyo.

Shukrani za pekee ziwaendee madaktari, wauguzi na jumuia nzima ya Agakhan Hosp alipolazwa Arthur baada ya kuzaliwa na kabla ya kifo chake. Paroko, Masista na watoa huduma wote wa Kanisa Katoliki la Mt. Immaculata Upanga kwa huduma za kiroho hasa ubatizo na mazishi. Wafanyakazi wenzake Bw. Francis Kassidi na Bibi Clara Kassidi. Ndugu, Jamaa na Marafiki wote kwa ujumla.

Ni vigumu kutaja watu wote kwa majina, lakini tunaomba mpokee shukrani zetu za dhati kwa hali, mali na moyo wa imani mliouonyesha wakati wa kutufariji katika kipindi chote kigumu mpaka sasa.

Tunasema Ahksateni sana. KICHWANGUMU

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.