Msiba...

Kwa masikitiko makubwa, napenda kuwataarifu wadau na wanajamii wote kwa ujumla kwamba familia ya Bw. Francis na Bi. Clara Kassidi wa Sinza dar es salaam wamepoteza mtoto wao mchanga, aliyezaliwa jumamosi iliyopita (18th July 2009) na kufariki alfajiri ya kuamkia leo (23rd July 2009) kwa matatizo ya kupumua.

Kutakuwa na misa ya kumwombwa marehamu leo (alhamisi 23rd July 2009) saa 8:30 mchana katika kanisa katoliki la Mt. Immaculata, Upanga. Baada ya hapo waombelezaji na wafiwa wote kwa ujumla wataelekea Kinondoni makaburini (makaburi ya ndani) kwenda kuuhifadhi mwili wa kichanga wetu.

Baada ya mazishi, wale watakaopenda kwenda kuwafariji wazazi na ndugu wanakaribishwa nyumbani kwa Bw. na Bibi Kassidi, Sinza Makaburini (kwa upande wa Shekilango Rd) au Sinza Super Star (kwa upande wa Sam Nujoma Rd).

Ahksanteni sana, tunaomba ushirikiano wenu.

Kwa niaba ya blogu hii ya jamii, familia yangu na mimi mwenyewe nawapa pole sana wazazi na ndugu wote kwa kufikwa na msiba huu. Poleni sana, tunaamini yote yaliyotokea ni kwa mapenzi ya Mungu.

Tunamwomba Mwenyezi Munghu amlaze mahali pema peponi kichanga wetu, amen.Bwana ametoa, na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. KICHWANGUMU.

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.