Maiti 13 za wanaodhaniwa abiria wa ajali ya ndege ya comoro waopoloewa kisiwani Mafia

Zimepokelewa taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Manzie Manguchie kuwa maiti 13 wanaodhaniwa kuwa ni wa ajali ya ndege iliyoanguka kutoka visiwa vya Comoro hivi karibuni wamepatikana katika fukwe za kisiwa cha Mafia katika mkoa wa Pwani.

Sambamba na maiti hao, yamepatikana pia mabaki ya mabati yanayosadikiwa kuwa ni ya ndege. Baadhi ya mabati hayo yameandikwa “Airbus 310, 1990”.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kati ya maiti waliopatikana katika maeneo
mbalimbali ya fukwe za Mafia hadi saa 11 jana (Jumanne, Julai 7, 2009) jioni,
maiti 11 wanaonekana kuwa ni Wazungu na maiti wawili ni Waafrika.

Kwa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Comoro na
Ubalozi wa Ufaransa, wamejulishwa taarifa hizo.

Wananchi wa Mafia na maeneo mengine wametakiwa kupiga ripoti haraka kwenye Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa na au Polisi, wakiona maiti au vyuma na mabati wanayoyatilia mashaka baharini au popote pale.

Ofisi ya Waziri Mkuu imeipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia na
wananchi wa Mafia kwa jumla kwa kazi ya kubaini maiti na mabaki hayo ya
ndege na kupiga ripoti.

Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021,
DAR ES SALAAM

Comments

Popular posts from this blog

FAMILIA YANGU ILIPOTEMBELEA KIJIJI CHA WATOTO YATIMA CHA FURAHA MBWENI KINACHOSIMAMIWA NA MASISTA WA KATOLIKI WA SHIRIKA LA KIMISIONARI LA BIKIRA MARIA MAMA WA YATIMA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17 JANUARI 2016

Rest In Peace Son of Africa, Meles Zenawi.