janet na john siku ya sherehe ya kupokea kipaimara



tukio:
katika mlolongo mzima wa sherehe hii, janet na john waliomba kusoma risala, katika risala hizo waliwashukuru wazazi wao na kuwaomba waendelee kuwasomesha ili waje kupata maisha bora. risala ya john iliwatoa watu machozi kwa sababu asilimia kubwa pale ukumbini hawakujua kama john ni yatima. ilimlazimu mama yake mlezi (vale) kwenda kuweka msisitizo baada ya risala huku akilia, kwamba hawakuwatuma (yeye na mumewe) na wala hawakujua yaliyokuwepo kwenye risala husika. kilikuwa kipindi kigumu kwa wengi waliokuwepo ukumbini, mama yake mkubwa john (dada yake vale) naye aliipokea risala huku akilia... ilisikitisha sana. tunawaombea wazazi walezi wa john (joseph na vale) Mola awazidishie na kuwawezesha watoto hao wasome.
Comments